Katibu Mkuu wa Sekta
ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho akifafanua jambo kwa viongozi mbalimbali wa
sekta ya uchukuzi (hawapo pichani), katika Mkutano wa Sita wa Kamati ya
Mawaziri wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi uliofanyika jijini Dar es
salaam. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa.
Katika
kuunganishwa na nchi ya Rwanda na Burundi, Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa
reli hiyo itajengwa kuanzia Isaka-Rusumo mpaka Kigali na Keza mpaka Musongati.
Naye
Waziri wa Uchukuzi wa nchi ya Burundi Eng. Jeon Ntunzwenidana amefurahishwa na
Serikali ya Tanzania katika jitihada zake za kuharakisha ujenzi wa reli hiyo na
amesema Serikali ya Burundi itakamilisha ujenzi huo haraka ili kurahisisha
usafirishaji wa mazao na huduma za kibiashara baina ya nchi hizo.
Waziri
Prof. Mbarawa amesaini makubaliano ya uboreshwaji wa sekta ya mawasiliano, reli
na barabara baina ya nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya
Demokrasia ya Congo (DRC).
Zaidi
ya trilioni 16 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa reli ya kisasa nchini Tanzania
yenye takribani urefu wa KM 2,600.
|
Post a Comment