Header Ads

Orodha ya Wagombea Nafasi ya Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi CUF Hii Hapa

  

Wagombea Uenyekiti Taifa:
NO.
JINA KAMILI
UMRI
JINSIA
ELIMU
MAFUNZO YA KITAALAM
1
Abdul Omari Zowo
66
ME
Secondari
Enginearing ndege za Kivita China na Urusi
2
James Kija Mahangi
42
ME
Sekondari
Upimaji wa magonjwa ya Binaadamu (MAABARA)
3
Joseph Magoiga Rhobi
48
ME
          -
Ufundi Seremala
4
Juma Shabani Nkumbi
49
ME
Secondari
Computer Course
5
Riziki Shahari Mngwali
56
KE
Chuo kikuu
Usuluhishi wa Migogoro
6
Salum Khalfan Barwany
57
ME
sekondari
Ufundi Magari
7
Selemani Khatibu
37
ME
Sekondari

8
Twaha Issa Taslima
63
ME
Chuo Kikuu
Sheria
9
Zuberi Mohamed Kuchauka(MB)
54
ME
Chuo
F.T.C. Mechanical
Wagombea Makamo Uenyekiti Taifa:
NO.
JINA KAMILI
UMRI
JINSIA
ELIMU
MAFUNZO YA KITAALAM
1
Dr. Juma Amer Muchi

ME
Chuo Kikuu
Afya
2
Juma Duni Hajji

ME
Chuo Kikuu
Uchumi
3
Mussa Hajji Kombo

ME
Sekondari

4
Salim Abadalla R. Bimani

ME
Chuo



Waheshimiwa Waandishi wa habari, kwa niaba ya Chama Cha Wananchi CUF  Juni 2, 2016 CUF kiliitisha kikao na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Shaaban Khamis Mloo kwa lengo la kuelezea kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Chama wa taifa ambao ungetumika kujaza nafasi mbalimbali za uongozi zilizo wazi.

Tulieleza kwamba nafasi zilizo wazi ni ya Mwenyekiti wa taifa wa Chama na hii imetokana na aliyekuwa Mwenyekiti wetu Profesa Ibrahim Lipumba kuamua kujiuzuru mwenyewe katika nafasi hiyo mnamo tarehe 5 August 2015, pia nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa taifa iliyotokana na Mheshimiwa Juma Duni Haji kujiuzuru nafasi hiyo na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili aweze kuwa mgombea Mwenza wa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Mheshimiwa Edward Lowassa aliyeungwa mkono na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

Nafasi nyingine zilizowazi ni pamoja na nafasi nne za Ujumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la taifa  kwa Kanda zifuatazo, idadi na aina na wajumbe wa kuchaguliwa katika mabano: Nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini (Mjumbe yeyote wa Kanda hiyo anaweza kugombea), nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Kati (Mjumbe yeyote wa Mkutano Mkuuu taifa kutoka Kanda hiyo anaweza kugombea, nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Ziwa (ni Mjumbe mwanamke tu kutoka kanda hiyo anaweza kugombea) na nafasi moja kutoka Kanda ya Kaskazini (mjumbe yeyote kutoka Kanda hiyo anaweza kugombea.

Katika ratiba ya matukio kuelekea siku ya Mkutano Mkuu maalum wa taifa tulieleza kwamba uchukuaji wa fomu za kuomba nafasi za kugombea utafanyika kwa Makatibu wa wilaya na kwamba siku ya mwisho ambayo Makatibu wa wilaya watapaswa kuwasilisha taarifa za waliogombea pamoja na fomu zao kwa Katibu Mkuu ni tarehe 10 August 2016.

No comments

Powered by Blogger.