Header Ads

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam PAUL MAKONDA azungumza na Kikosi cha FFU Ukonga

Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) ukonga Jijini Dar es Salaam, ambapo amewataka kutambua kwamba hakuna watumishi wazalendo kama Askari.

Makonda aliongezea kwa kusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu.

amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba waifanye dar es Salaam iwe kama dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta. 

Amesema anaamini Dar es Salaam inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa. 

-
Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt.John Magufuli, 

ombi la Makonda lilikua juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika bila kuchelewa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU katika Kambi yao iliyopo eneo la Ukonga.

No comments

Powered by Blogger.