Marufuku ya Bibi na Bwana Shamba Kukaa Ofisini yatolewa Wilayani KILOLO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Bw
Aloyce Kwezi akiwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Bi Asia Abdalah
katika viwanja vya nane nane jijini Mbeya mara baada ya waziri mkuu kumaliza kufunga maonyesho hayo.
Serikali ya wilaya
ya Kilolo mkoani Iringa
imewaagiza mabwana na mabibi shamba
katika halmashauri hiyo kutoka
maofisini na kwenda mashambani
kuwasaidia wakulima kulima kisasa ili kuongeza uzalishaji wa mazao.
Mkuu wa wilaya ya
Kilolo Bi Asia Abdalah aliyasema
hayoa wakati wa kilele cha maonyesho
ya wakulima (nane nane )
kwenye banda ya Halmashauri ya
wilaya ya Kilolo
wakati wa kufunga maonyesho hayo juzi.
Alisema kuwa pamoja
na wilaya yake kuonyesha ushiriki mzuri wa maonyesho hayo na wananchi wengi
kufika kujifunza katika
banda la
Kilolo namna ya kilimo bora chenye
tija ila alisema bado
wao kama Kilolo kwa kushirikiana na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw
, Aloyce Kwezi
pamoja na wataalam wote hasa
wale wa kilimo kufanya kazi kama timu
ili kuwasaidia wakulima wa
Kilolo kusonga mbele
Mkuu huyo
alisema kuwa kati ya wilaya zinazoongoza
kwa kilimo cha mahindi
na mazao mengine ya biashara ndani ya
mkoa wa Iringa ni pamoja na wilaya hiyo ya
Kilolo hivyo alisema iwapo kila
mtaalam wa kilimo atawajibika kwa nafasi yake kauli mbiu ya Rais Dr John Magufuli ya Hapa Kazi
tu inaweza kuwasaidia
wananchi kuongeza kasi ya
uzalishaji .
Kwani alisema pamoja na
jitihada kubwa zinazofanywa
na wataalam hao
wa kilimo katika wilaya ya
Kilolo katika kuwasaidia wakulima ila bado zipo changamoto kiasi kwa
baadhi ya wataalam wa kilimo
kutotimiza wajibu wao .
“ Lengo ni
kuona kila bwana shamba ama
bibi shamba kwa maana ya wataalam wa ugani wote
wanatimiza wajibu wao kwa kutoka maofisini na kwenda mashambani walikowakulima ili
kuwasaidia kuongeza kasi ya uzalishaji zaidi”
Hata hivyo
alisema iwapo wataalam wa
kilimo watakwenda kwa wananchi na kushinda nao mashamani upo uwezekano
wa wilaya ya Kilolo kwa maonyesho yajayo kushika nafasi ya kwanza kikanda na kuwa na
wakulima wenye kasi kubwa ya uzalishaji
.
Pia alisema moja kati ya majukumu ambayo yametolewa na waziri
mkuu wakati wa ufungaji wa
maonyesho hayo ni pamoja na kusimamia kasi ya uzalishaji na kuwa
kwa wilaya ya Kilolo suala
hilo linawezekana kusimamiwa na
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa .
Huku kwa upande
wake Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya Kilolo Bw Aloyce Kwezi alisema kuwa wilaya hiyo iaongoza kwa kilimo
cha nyanya ,vitunguu na mahindi pamoja na mazao mengine na
kuwa uwezekano wa wananchi wa
Kilolo kufanikiwa kiuchumi
upo mkubwa iwapo kila mmoja
atatimiza wajibu wake .
Alisema zao la nyanya
limekuwa ni ukombozi mkubwa kwa
wananchi wa Ilula kama ilivyo zao la vitunguu kwa
waanchi wa Nyanzwa na kudai
hadi sasa serikali imeendelea kuwasaidia
wakulima hao katika kuboresha skimu
za umwagiliaji katika maeneo ya
Mtandika , Ruaha mbuyuni na Nyanzwa na
kuwa kupitia skimu hizo
wananchi wameweza kuongeza uzalishaji .
MWISHO
Post a Comment