Makamu wa Rais SAMIA SULUHU afanya Mazungumzo na Taasisi ya HANS SEIDEL
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya HANNS SEIDEL kutoka nchini
Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto)ambaye ameongoza ujumbe wa watu
wanne akiwemo Waziri wa Nchi, Kazi, Masuala ya Kijamii wa Bavaria
Mhe. Emilia Muller walipometembelea Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Shirikaka la HANNS SEIDEL kutoka nchini
Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto) pamoja na Waziri wa Nchi,
Kazi, Masuala ya Kijamii wa Bavaria Mhe. Emilia Muller
walipometembelea Makamu wa Rais Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
(katikati)
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Taasisi ya HANNS
SEIDEL la Ujerumani,Wengine pichani ni Waziri wa Nchi, Kazi, Masuala ya
Kijamii wa Bavaria Mhe. Emilia Muller ( kulia) Mwenyekiti wa Taasisi ya
HANNS SEIDEL kutoka nchini Ujerumani Profesa Ursula Mannle (kushoto),
Mwakilishi Mkazi wa Taasisi HANNS SEIDEL Bi. Julia Berger( wa pili
kushoto),Meneja wa Mradi Kadele Mabumba (wa pili kulia), Ikulu
jijini Dar es Salaam
..............................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameitaka Taasisi
ya Hans Seidel Foundation isaidie kupeleka Elimu ya Uraia bungeni ili wabunge
wajue wajibu wao ndani na nje ya Bunge.
Mhe.
Samia ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana na ujumbe wa Taasisi ya Hans
Seidel Foundation uliomtembelea ofisi kwake Ikulu, Jijini Dar es salaam kutaka
kujua kama ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna sheria na
kanuni za kuendesha vikao vya Bunge.
Makamu
wa Rais aliueleza ujumbe huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa Hans Seidel
Foundation Prof. Ursula Mannle kuwa sheria na kanuni zipo za kuendesha vikao vya
Bunge lakini baadhi ya wabunge hawazifuati kama inavyotakiwa.
Alisema
kwa mtazamo wake elimu ya uraia itasaidia katika kuwafanya wabunge hao wajenge
nidhamu katika michango na ushiriki wao kwa ujumla ndani na nje ya Bunge.
Akizungumzia
kuhusu kuanzishwa kwa dawati la jinsia katika vituo vya polisi Mheshimiwa Samia
alisema ni hatua nzuri kwani wanawake kwa sasa wako huru kueleza wanapofanyiwa
ukatili wa kijinsia tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
"Kwa
sasa wanawake wanakutana na wanawake wenzao wako huru kuzungumza wanaporipoti
matukio ya kupigwa na haki inatendeka bila ya hata kutoa rushwa.
Kuna mabadiliko
ndani ya Jeshi la Polisi kwa upande huo," alisema Mhe. Samia.
Alisema
kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha watu wote
wanaoenda kinyume na taratibu wanachukuliwa hatua za kisheria na kusema kwenye
utumishi wa umma mambo yamebadilika kiasi kwamba makusanyo ya kodi yameongezeka Serikalini.
Taasisi
ya Hans Seidel Foundation yenye makao yake makuu Munich, nchini Ujerumani
ambayo inajishughulisha na masuala ya demokrasia, amani na maendeleo huku
ikitoa kipaumbele kwenye elimu ya uraia inaendesha shughuli zake katika nchi
zaidi ya 60 duniani.
Post a Comment