Katika hali isiyo ya
kawaida shirika la maji safi na maji taka DAWASCO jijini Dar Es Saaal na Pwani
DAWASCO, limeingia mitini
katika Ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina ya
kutembelea miondombinu ya maji taka na
maji safi Jinini dar Es Salaam na Pwani Leo.
Licha ya Shirika Hilo kupewa Taarifa ya Ziara ya Naibu waziri
Mpina mwezi mmoja kabla limekaidi kwa kutoitikia wito huo hata kwa
kumuwasilisha mtumishi mmoja kuwakilisha shirika hilo.
Akiongea kwa ukali baada ya kutembelea Bomba la kusafirisha
maji taka kwenda baharini la Ocean road, Naibu Waziri Mpina amesema ubovu wa
bomba la ocean road unatokana na kutokukarabatiwa kwa muda mrefu, unaonyesha
dhahiri kuwa DAWASCO wana Jeuri kwa IKulu, kwa kutokulifanyia ukarabati kwa
muda muda mrefu Bomba hilo lililoko karibu na maeneo hayo.
|
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina
akiwa katika ziara ya kukagua uharibifu wa mazingira.
Alipotembelea mabwawa ya maji taka ya mabibo na buguruni, Mhe
Mpina Alisema pamoja na kuwa miondombinu hiyo inaelemewa na wingi wa wakazi wa Dar Es Salaam, Mamlaka husina zina
wajibu wa kuyafanyia usafi mabwawa hayo lakini, hazijaonekana jitihada zozote
za kufanya hivyo, na miondombinu hiyo inaonekana kutofanyiwa ukarabati kwa muda
wa miezi sita.
Naibu Waziri Mpina alisisitiza kuwa ubovu na uchafu wa
miundombinu hiyo unapelekea uchafuzi wa mazingira na hivyo kuhatarisha maisha
ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na viumbe hai wengine.
Akiongea kwa Uchungu, Mkazi mmoja wa Mabibo aliyekataa kutaja
jina lake alisema kuwa, ninanukuu“Mabwawa
haya ni ya Dawasco na hata tukitaka kuunganisha maji taka kwenye mabomba yao
kuelekea kwenye mabwawa wana taka tuwalipe na tunafanya hivyo, wenye viwanda
halikadhalika wanawalipa dawasco kwa kupitisha maji taka yao katika miundombinu
ya dawasco, lakini najiuliza, kwa nini wanakuwa wagumu kuyafanyia ukarabati au
hata kusafisha tuu?. Mwisho wa kunukuu.
|
|
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina
akisikiliza kero za harufu kali za mabwawa ya maji taka kutoka kwa wana nchi
yaliyopo Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara
ya ukaguzi wa mazingira. |
|
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara kukagua miundo
mbinu ya Dawasco inayolalamikiwa na wana nchi kwa kutiririsha maji machafu sehemu za makazi, jijini Dare s salaam mapema
hii leo.
Ziara ya Naibu waziri Mpina ya kukagua miundiombinu ya
DAWASCO leo Jijini Dar Es Saalam ilihushisha maafisa kutoka DAWASA na BAraza la
taifa la hifadhi ya Mazingira NEMC na kuwaagiza NEMC, wapitie miradi yote
inayosimamiwa na DAWASCO na kuon akama wanatenda haki katika kutoa huduma kwa
wananchi.
|
Post a Comment