UNIDO yaendesha Mafunzo kwa Wamiliki wa Viwanda Vidogo Vidogo vya Uzalishaji (SMEs)
Na Mwandishi Wetu
Shirika la Umoja wa
Mataifa linalohusika na maendeleo ya
viwanda UNIDO kwa kushirikiana na Chuo Kikuu
cha Mzumbe wameendesha semina kwa
wahitimu kutoka vyuo mbalimbali pamoja na viwanda vidogo vidogo,
wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo wadogo
Jijini Dar es salaam.
Akitoa maelezo katika
semina hiyo Mkuu wa Chuo Kampasi ya Mzumbe Dar es salaam Profesa Ganka Nyamsongoro alisema lengo kubwa
la kutoa semina hiyo ni kuwaalika vijana
pamoja na wenye viwanda vidogo vigogo kujiunga katika programu utakaoendeshwa na UNIDO kwa kushirikiana na
Mzumbe.
"Lengo kubwa la programy
hiyo ni kutoa fursa kwa vijana ambao
wamehitimu katika vyuo mbalimbali kuweza kufanya kazi kwa vitendo kulingana na
taaluma zao pamoja na kufanya kazi na wenye viwanda vya kati na kuendesha
miradi midogo midogo ili kukuza kipato chao pamoja na kuleta maendeleo kwa Taifa" alisema Profesa Nyamsongoro
Wakizungumza kwa
nyakati mbalimbali wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalisjaji,
wafanyabiashara na wajasiliamalia mali wamesema kuwa hii ni fursa muhimu kwao
na watakuwa tayari kuwasaidia vijana hao wahitimu ambao wanategemea kuwa nao
katika mafunzo ya kazi.
Kwa Upande wake Profesa
Honest Ngowi ambaye ndiye msimamizi wa programu alisema UNIDO wakishirikiana na
Chuo Kikuu cha Mzumbe watakuwa na waangalizi mbalimbali watakao zunguka
kuangalia utendaji kazi wa vijana hao wakiwa kwenye programu hiyo.
Kwa upande wake
‘mentor’ wa programu hiyo Bwana Kaaya amewataka vijana wanaohitimu vyuo vikuu
umuhimu wa kuweza kutumia taaluma zao katika Nyanja mbalimbali hasa kwa kutumia
fursa zilizopo na kuweza kujiajiri.
Mchangiaji mwingine
katika semina hiyo Bw. Deosdadit Bernard ambaye ni msimamizi wa programu hiyo kutoka UNIDO alisema programu utaendeshwa kwa muda wa
miezi minne na mwishoni watakaofuzu
watapewa barua za utambulisho ili iweze kuwa rais kuajirika katika
maeneo mengine kwa Urais.
Aidha mtoa mada
Dr.Darleen Mutalemwa aliwashukuru UNIDO Chuo cha Mzumbe pamoja na kwa mchango wao
katika jamii ,na amewataka wahitimu na wenye viwada vya kati na kuwataka
kutokata tama na washiriki vyema katika programu hiyo kwani utatoa nafasi yaw o
kuweza kuimarika katika soko la ajira.
Hata hivyo bado watu
wenye viwanda vidogo vigogo vya uzalishaji na wajasiriamali pamoja na wahitimu
wa vyuo vikuu wanahitajika katika kuomba nafasi ambazo bado zipo wazi kupitia
katika tovuti ya www.dcc.mzumbe.ac.tz
Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam Profesa Ganka Nyamsongoro akifungua Semina kwa ajili ya wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara na wajasiliamali semina iliyolenga programu ya UNIDO wakishirikiana na Chuo kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kupata mafunzo ya ujuzi wa kazi.
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Peacock Hotel Dar.
Mshauri wa UNIDO Bw. Mike Laizer akichangia jambo katika semina hiyo.
Bw. Deosdadit Bernad Msimamizi wa Programu kutoka UNIDO akielezea kwa undani juu ya Programu hiyo.
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiendelea kufuatilia Semina.
Profesa Prosper Ngowi Msimamizi Mkuu wa Programu hiyo akieleza kwa kina nia na malengo ya wao kufanya hivyo kwa kushirikiana na 'SMEs' ili kuwapa ujuzi wa kazi wahitimu na wahitimu kutoa ujuzi wao waliokuwa nao ili kuweza kukuwa zaidi.
Wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanaendelea kufuatilia semina hiyo kwa makini.
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiwa wanauliza maswali na kuchangia mawazo katika Semina hiyo.
Mmoja wa 'Mentor' katika programu hiyo Bw. Kaaya akiwa anatoa maelezo kwa wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali jinsi ambavyo watashirikiana katika kuwafundisha kazi wahitimu hao pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali.
Picha ya Pamoja kati ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali, Chuo kikuu cha Mzumbe na wawakilishi kutoka UNIDO.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Profesa Ganka akifungua semina fupi na wahitimu kutoka vyuo mbalimbali ambao ni watanzania katika programu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe juu ya Mafunzo ya kazi 'Internship' ambayo yataanza hivi karibuni ambapo wahitimu hao watatakiwa kufanya kazi kwa miezi minne katika viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara na wajasiliamali.
Msimamizi Mkuu wa Programu kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Prosper Ngowi akiwaelezea wahitimu juu ya Programu hiyo.
Baadhi ya wahitimu wakiwa wanauliza maswali na kutaka ufafanuzi katika baadhi ya maeneo ambayo walikuwa hawajayaelewa katika semina hiyo iliyofanyika katika Chuo kikuu cha Mzumbe.
Dkt. Darleene Mutalemwa akitoa neno la Shukurani kwa wote wahitimu wote waliofika katika semina hiyo kwa niaba ya UNIDO na Chuo kikuu cha Mzumbe.
Wahitimu wakiwa katika semina hiyo ya kupata maelekezo juu ya Programu ambayo inalenga kuwapa Mafunzo ya kazi wahitimu iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo kikuu cha Mzumbe.
Post a Comment