Rais Dkt MAGUFULI amteua PAUL CHAGONJA na COLDWING MTWEVE kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ya KATAVI na MWANZA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu
Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala
wa mikoa hiyo.
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Kabla ya Uteuzi
huo, Kamishna Mtweve alikuwa
Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Balozi Sefue
amesema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa polisi Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda
kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni
Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Kabla ya Uteuzi
huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna
wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Aidha, Balozi
Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hawa wa Polisi
kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu
wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.
Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait,
wataapishwa kesho Jumamosi tarehe 30 Januari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam,
saa nne asubuhi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam.
29 Januari,
2016
Post a Comment