Chama cha Karate Mkoani KILIMANJARO waiomba Serikali Kutupia Jicho
Vero Ignatus - Moshi Kilimanjaro
Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro wanaiomba serikali kutupia macho kwenye mchezo huo kwani imekuwa ikiwasahau ukizingatia mchezo huo ni michezo kama ulivyo mingine na kwamba mchezo huo umekuwa ukifundishwa pia katika majeshi mbalimbali hapa nchini.
Hayo yamesemwa nakapteni wa timu na katibu msaidizi wa chama cha Katrate mkoa wa Kilimanjaro bwana Wembo Hamisi katika viwanja vya mazowezi mkoani hapo na amekusema kuwa wamekuwa wakikwama mara wanapohitajika kwenye mechi za kirafiki,ndani na nje ya nchi kwasababu hawana sapoti kutoka serikalini na wafadhili.
Aidha amesema kuwa Karate ni mchezo ambao mtu yeyote anaweza kuucheza na akatengeneza afya ya mwili,na mchezo huo ni wa kawaida kama ilivyo michezo mingine kama mpira wa miguu amewataka watu wote kujitokeza kwa wingi kujiunga katika mchezo huo wa Karate kwa sifa kuu ya karate ni nidhamu.
Sambamba na hayo bwana Wembo amesema kuwa katika mchezo huo wapo wanawake na ameiomba jamii waondokane na ile dhana potofu kwamba mwanamke akicheza mchezo huo wa Karate hawezi kupata mtoto na kufanya shughuli nyingine za kijamii amesema huo ni upotoshaji kwani mwanamke anao uwezo wa kupata mtoto kama walivyo wengine na anatengeneza afaya nzuri kabisa.
Aidha amesesema kuwa mchezo huo wa Karate kwa historia umeanzishwa miaka mingi kwa mkoa wa Kilimanjaro chama cha karate kina takribani miaka saba sasa tangia kuanzishwa kwa chama hicho,na baadae wakaunda shirikisho la Karate nchini Tanzania ambapo inajumuisha michezo yote ya karate ,ambapo januari 30 watakuwa na tamasha la Karate la kuwatambulisha wachezaji wa timu litakalofanyika mkoani hapo katika ukumbi wa shule ya msingi Mwenge.
Katibu huyo ameinisha ratiba yao ndani ya miezi sita ambapo watafanya matamasha mbalimbali ikwemo februari 13/2016 watafanya tamasha wilayani Same katika ukumbi wa kimweli same mjini, machi 24-26, mashindano ya mchezo wa GOJUKAI KARATE ya Afrika Mashariki, Kampala Uganda , aprili 30 mashindano ya GOJUKAI Karate ya wazi ya kuuenzi mlima Kilimanjaro ambapo watashiriki watoto wenye umri wa kati na watu wazima yatafanyika Moshi, Mwisho ni Tamasha la shukrani litakalofanyika mei 16 hapo hapo Moshi Kilimanjaro.
Kwa mkoa wa Kilimanjaro mchezo wa karate unaochezwa unajulikana kama Gojukai Stayle, ambayo ilianzishwa kutoka nchini Japan,na chama katika mkoa huo kinaundwa na vilabu mbalimbali ambavyo klabu mama ni Ralway club, Pasua Club, Mwenge Club, Ccp Club,Rau Club,na vilabu vingine vinaundwa na wanafunzi mbalimbali ambapo kila club ina zaidi ya wanafunzi 20-30.
hivyo wanawaomba ,Taasisi mbalimbali ,wafanyabiashara,makampuni mbalimbali hata watu binafsi kujitokeza kuudhamini mchezo huo wa Karate.
Post a Comment