SERIKALI YAJA NA MIKAKATI MIPYA YA KUHAKIKISHA UTALII WA NDANI UNAKUA
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi akisisitiza jambo wakati alipokuwa
anamkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja.
Generali. Gaudence Milanzi kufungua Mkutano Mkutano wa Kamati ya
Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika leo
Mpingo House jijini Dar es Salaam wa kujadili changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya Utalii nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Meja. Generali. Gaudence Milanzi ( kulia) akiwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Deogratius Mdamu (kushoto)
wakimsikiliza Mjumbe ( hayupo pichani ) wakati wa Mkutano wa Kamati ya
Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) uliofanyika leo
Mpingo House jijini Dar es Salaam akiwa anazungumzia changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini na kutoa ushauri ya
namna kuuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa bado ni changamoto kwa
wananchi wengi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya
Uwezeshaji Utalii ( Tourism Facilitation Committee- TFC) wakiwa
wanajadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii nchini
kwa kutoa maoni, ushauri na ufumbuzi wa changamoto ikiwa na kuchangia
mikakati mbalimbali itakayowezesha kusaidia kuhamasisha Utalii wa ndani.
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Wakati nchi nyingi Afrika zikiwa zinafanya jitihada mbalimbali
za kuimarisha Utalii wa ndani ambao umekuwa ndo wa uhakika katika
kuiingizia nchi mapato hata pale majanga yanapotokea, Nayo Tanzania
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuhakikisha kuwa Utalii
wa ndani unakua kwa kasi inayotarajiwa.
Baadhi ya Majanga hayo yanayoathiri Sekta ya Utalii ni milipuko
ya magonjwa kama Ebola, matukio ya Ugaidi Kenya na kushuka kwa Euro ya
Ulaya dhidi ya Dola ya Marekani.
Hivyo Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau
wa Utalii nchini wamepanga mikakati ya kuhakikisha kuwa Utalii wa ndani
unakuwa tegemeo tofauti na sasa ambapo Watalii kutoka nje ndio wamekuwa
wamekuwa wakitembelea hifadhi zetu kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza kwenye Mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Utalii
ijulikanayo kama Tourism Facilitation Committee ( TFC) uliofanyika leo
Mpingo House jijini Dar esSalaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili,
Meja. Generali. Gaudence Milanzi na Utalii amesema maendeleo ya Utalii
yanahitaji sana Utalii wa ndani kuimarika baadala ya kudhani kuwa
vivutio vya utalii vilivyopo ni kwa ajili ya wageni kutoka nchi za nje.
Meja. Generali. Milanzi amesema Utalii ni sekta nyeti sana
katika kuliingiza Taifa pesa za kigeni lakini hata hivyo ni sekta ambayo
imekuwa inaathirika kwa haraka sana pindi majanga yanapotokea nchi
jirani hivyo ni lazima jamii ijengewe utamaduni wa kutembelea vivutio
vya Utalii ili kuweza kujihakikishia Watalii wa ndani wanakuwa wengi.
Baadhi ya mikakati iliyopendekezwa na Wajumbe wa kamati ya
Uwezeshaji Utalii (TFC) ni kuwawezesha maafisa Utalii wa Halmashauri
wanatengewa bajeti ya kutosha, wanajengewa uwezo kuhusu ya vivutio vya
utalii vilivyopo kwenye maeneo yao pamoja na Idara ya Utalii kufungua
ofisi kila kanda ili kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Aidha,viwanja vya ndege vilivyopo nchini viimarishwe ikiwa
pamoja na nchi kuwa ndege zake kama ilivyo kwa nchi jirani kama Kenya na
Rwanda
Awali , Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,Bi. Uzeeli Kiangi
alisema Mkutano wa TFC hutoa fursa za kuziibua na kujadili changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta ya Utalii hivyo Sekta Binafsi zinawajibu
mkubwa wa kuhakikisha changamoto zinazoikabili sekta zinatafutiwa
ufumbuzi
Aliongeza kuwa Idara ya Utalii imekuwa ikishiriki katika
maonesho mbalimbali ya kitaifa lengo likiwa ni kutoa elimu kwa jamii
kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya Utalii nchini.
Aidha, Prof Wineastor Anderson amesema sekta ya Utalii imekuwa
inakua lakini si kwa kiwango cha kuridhisha hivyo jitihada za kutangaza
utalii ndani na nje nchi upewe uzito unaostahili kwa kuiwezesha Bodi ya
Taifa ya Utalii inatengewa bajeti ya kutosha.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii
Tanzania ( TCT) Bw. Richard Rugimbana, amesema Utalii wa ndani ili uweze
kukua suala la elimu linahitajika kutolewa ili kuweza kuibadilisha
jamii ipende kutembelea vivutio vya Utalii.
Naye Kamanda wa Polisi Jk Ndaki anayeshghulikia dawati la Utalii
( Tourism Police Unit) amewahakikishia usalama wao watalii wa ndani na
nje ya nchi kutembelea vivutio vya Utalii bila hofu yoyote kuwa Jeshi la
Polisi nchini lipo macho muda wote.
Post a Comment