Shirika la TANESCO limelalamikiwa na Mteja Kwa Kuchelewa Kutoka Huduma
Mteja Ambwene Kyoga |
Dotto Mwaibale
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Charambe Temeke jijini Dar es Salaam limelalamikiwa na mteja wake mmoja kwa kushindwa kumfungia umeme kwa wakati licha ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo kuagiza wateja wapya kufungiwa umeme katika kipindi kifupi.
Malalamiko hayo yametolewa na mteja wa shirika hilo Ambwene Kyoga ambaye amelipa sh. 320,960 kwa ajili ya kuwekewa umeme na kupatiwa lisiti namba TDB 16841 kwa ajili ya nyumba yake iliyopo Mbagala Kuu Bucha.
Ambwene alisema sasa anaingia mwaka wa pili bado haja fungiwa umeme kwani mwaka jana mwanzoni alipeleka maombi yake ofisi za shirika hilo za Kurasini lakini alipofuatilia aliambiwa faili lake limepotea hivyo aende ofisi za Charambe ambapo alilipa fedha hizo Desemba 28 mwaka jana tangu hapo licha ya kupelekewa nyaya amekuwa akizungushwa kwa kuambiwa nguzo inayotakiwa achukulie umeme imeoza ingawa inaendelea kutumika.
"Watu wa dharura wamekwisha toa taarifa kuhusu nguzo hiyo lakini bado haijabadilishwa jambo linaloweza kuleta maafa iwapo ikianguka na kibaya zaidi wamekuwa na maneno mengi badala ya kazi sijui wanataka kujenga mazingira ya rushwa" alilalamika Kyoga.
Kyoga alisema waziri wao Mhongo anafanya kazi kwa kujituma na alimsikia katika vyombo vya habari akiagiza kuwa ndani ya wiki moja mwombaji wa umeme awe amefungiwa lakini anashangaa Tanesco Charambe jinsi wanavyofanya kazi kwa kusuasua.
Msemaji wa Tanesco ofisi za Charambe ambaye alifahamika kwa jina moja la Mugaya alipopigiwa simu jana ili kuzungumzia suala hilo simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila ya kupokewa hata hivyo gazeti ili linaendelea kumtafuta.
Post a Comment