Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili akutana na Kundi la Washirika wa ( DPG-E )
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi (kulia) akizungumza na viongozi wa Kundi la Washirika wa Maendeleo katika sekta ya Mazingira, Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Development Partners Group on Environment, Natural Resources and Climate Change (DPG-E) walipoonana leo tarehe 19 Januari, 2016 katika ukumbi wa Selous uliopo makao makuu ya Wizara hiyo Mpingo House. Kundi hilo liliomba kuonana na Katibu Mkuu huyo kwa ajili ya utambulisho na kujadili mambo muhimu ya maendeleo katika sekta hiyo.
Bi. Lena Thiede (kushoto) kutoka ubalozi wa Ujerumani ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Shirikisho la Kikanda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutoka Kundi la Washirika wa Maendeleo katika sekta ya Mazingira, Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi (DPG-E) akizungumza katika kikao hicho ambapo alielezea kazi ya Kundi hilo kuwa ni kuandaa mijadala maalum ya kisera na Serikali pamoja na wadau wengine wa maeneo husika, kuratibu miradi na mipango ya kundi hilo na kuhamasisha mawasiliano na utetezi wa pamoja baina yake na Serikali na wadau wengine katika sekta hizo. Katikati ni Bi. Clara Makenya kutoka UNEP ambaye ni Mratibu wa Kitaifa wa Kundi hilo na Bw. Steven Nyagondi Sekretarieti ya Kundi hilo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi (wa pili kushoto) akiongoza mazungumzo katika kikao hicho. Katika mazungumzo hayo Meja Generali Milanzi amewaomba wadau hao na wadau wengine wa Maliasili kuungana pamoja katika kuhifadhi Maliasili za Tanzania ikiwemo vita dhidi ya biashara haramu ya Maliasili za Taifa, Ujangili na uharibifu wa misitu. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Anjelina Madete.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Idara ya Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Zahoro Kimwaga, Bw. Herman Keraryo (katikati) Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori na Bw. Donatius Kamamba Mkurugenzi Idara ya Mambo Kale ambao wameshiriki katika kikao hicho.
Bwana Bernad Lubogo (kulia) Afisa Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii akichangia jambo katika kikao hicho, Wengine ni Bi. Bertha Nyange (Katikati) Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango na Bw. Joseph Sendwa Afisa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Maliasili na Utalii # www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)
Post a Comment