OJADAC walaani Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976
Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Chama
cha Waandishi wa Habari Wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu
Nchini OJADACT, Kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi yake
ya kufanyia marekebisho sheria kandamizi kwa vyombo vya habari nchini, aliyoitoa
wakati wa Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.
Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko, ametoa
ombi hilo hii leo mbele ya Wanahabari Jijini Mwanza, wakati akielezea hatua mbalimbali
ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali dhidi ya vyombo vya habari vinavyokiuka
sheria katika utendaji wake wa kazi.
Soko alitolea mfano Sheria ya Magazeti ya mwaka
1976 kupitia sura ya 229 kifungu cha 25 (1), kinachompa Mamlaka Waziri wa
Habari kulifungia gazeti lolote linalotoa habari zenye ukakasi, kuwa ni ishara
ya ukandamizaji wa uhuru wa habari nchini, kwa kuwa kuwa sheria hiyo haitoi
nafasi kwa chombo kinacholalamikiwa kujitetea ikizingatiwa kwamba Serikali
ndiyo mlalamikaji na wakati huo huo mtoa hukumu.
“Sheria ya Magazeti ni mbaya kwani haitoi nafasi
kwa upande wa pili kujibu, huku serikali ikiwa ndiyo mlalamikaji na hapo hapo
hakimu (Unfair game). Alitanabaisha Soko na kuongeza kuwa OJADACT inalaani
matumizi ya sheria ya magazeti nchini ya mwaka 1976.
Wakati OJADACT ikitoa ombi hilo kwa Rais
Dkt.Magufuli, baadhi ya Waandishi wa Habari Jijini Mwanza walikiri kuwepo kwa
sheria zenye ukandamizaji wa Uhuru wa habari nchini ambapo wameomba sheria hizo
kurekebishwa ili kukuza haki ya kutafuta na kutoa habari katika jamii.
Vyombo mbalimbali vya Habari nchini hususani
Magazeti, vimekuwa vikikabiliwa na sheria kadhaa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa
ya kwamba zinakiuka misingi ya uhuru wa habari ambapo ni hivi karibuni Serikali
imelifungia gazeti la Mawio kuchapisha habari zake kutokana na kuchapisha
taarifa zilizoelezwa kuwa na mkanganyiko katika jamii.
Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.
Wanahabari.........
Kulia ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG.
Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG.
Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG.
Baada ya Ojadact kutoa ombi lake kwa Mhe.Rais, Ikafuata Selfie.
Post a Comment