Uchaguzi wa Marudio ZANZIBAR sasa Kufanyika Machi 20 Mwaka huu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar imevunja ukimya leo hii mara baada ya kutangaza tarehe ya uchaguzi wa Marudio utakaofanyiwa visiwani humo tarehe 20 ya mwezi Machi Mwaka 2016.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Januari 2016 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha inaeleza kuwa kwa mujibu wa kikao chake kilichofanyika tarehe 21January 2016 imeamua kuwa Uchaguzi wa marudio utafanyika siku ya Jumapili ya Tarehe 20 Machi 2016.

Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais , Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ambapo kwa mujibu wa taarifa ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ( ZEC ) imesema kuwa hakutakuwa na uteuzi mpya wa Wagombea wala mikutano ya Kampeni, Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu.
Mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha ameomba wananchi visiwani humo kuendelee kudumisha amani na utulivu katika kipindi chote cha maandalizi, Siku ya kupiga kura, kuhesabu kura na baada ya kutangaza matokeo ya uchaguz huo.
Ikumbukwe kuwa Marudio ya uchaguzi visiwani Zanzibar yanafanyika mara baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Kusimamisha uchaguzi wa awali kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo matatizo ndani ya Tume hiyo ya uchaguzi na katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.
Post a Comment