Mtandao wa Tigo 4G LTE kupanuka Hadi Mji wa MOSHI
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo inaongoza kwa kuendesha maisha ya kidijitali
imetangaza mpango wake wakupanua huduma ya intaneti ya 4G hadi Moshi ifikapo Februari
mwakahuu. Huduma hiyo ilizinduliwa kwanza
jijiniDar es Salaam mwanzoni mwa mwaka
jana na baadaye ilisambazwa kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Dodoma na Morogoro,
kwa ufanisi na hivyo kuufanya mtandao wa
4G kuwa mpana na wakasi nchini Tanzania.
Ikichukuliwa
kama teknolojia nzuri ya hivi karibuni kwenye sekta Ya mawasiliano duniani isiyo
na dosari katika kuifikia huduma ya intaneti, teknolojiaya 4G LTE inakasi takribani
maratan ikilinganishwa na teknolojiaya
3G Ambayo inatumiwa na watoaji wengine wahuduma hiyo kwenye soko la Tanzania.
Akizungumza
kwenye mahoajiano maalum na vyombo vya habari kwenye ofisiza Tigo mjini Moshi pempezoni
mwa uzinduzi rasmi wa mbio za kila mwaka za masafa za Kilimanjaro Marathon,
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kusambazwa kwa mtandaowa 4G
kuna fanyika ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo wa kuwapatia wateja wake huduma ya
hali ya juu duniani ilikuwawezesha kuendesha
maisha ya kidijitali.
“Mpango
wa kupanua mtandao wa Tigo wa 4G hadi Moshi
kwa mara nyingine umeonesha sio tu kwamba Tigo inaongoza katika kutoa teknolojia
ya kisasa na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, balipia kujikita kwake Kuongeza kufikiwa kwa intaneti
kwaWatanzania wengi kadri iwezekanavyo,”alisema Wanyancha na kubainisha kuwa kuwalengo kubwa la kampuni hiyo ya simu ni kuhakikisha huduma hiyo inaenea nchi nzima ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2016.
Akizungumziambioza
Kilimanjaro Marathon ambazo Tigo ni mdhamini mwenza,Wanyancha alisema kwamba kama
kampuni ya maisha ya kidijitali aTigo imeamua Kuwaunga mkono wanamichezo wa umekwa wake hapa nchini ilikuwasaidia kufikia malengo yao
ya muda mrefu katika maisha.Wanyancha alihitimisha
kuwa tangu mwaka jana Tigo ilishawekeza dolamilioni
120 kwa mwaka kwenye upanuzi wa mtandao
wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao
ya 4G na 3G na mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima.
Post a Comment