Serikali imetumia Bilioni 459 Kukopesha Wanafunzi wa Elimu ya Juu Mwaka 2015 / 2016
Baadhi ya waandishi wa Habari
wakifuatilia mkutano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu na vyombo
vya Habari.
|
Frank-Mvungi-Maelezo
Serikali imetumia bilioni 459 kuwakopesha
wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi cha mwaka 2015/2016 ambapo jumla ya
wanafunzi 122,486 wamenufaika.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari
Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Omega
Ngole wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.
“Walionufaika na mikopo katika
kipindi cha 2015/2016 ni wengi na haijwahi kutokea katika Historia tangu
kuanzishwa kwa Bodi na haya ni matokeo
ya utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya tano “alisisitiza Ngole
Akizungumzia utolewaji wa mikopo Katika
kipindi cha mwaka 2014/2015 Ngole alibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 99,069
walipata mikopo na jumla bilioni 341 zilitolewa.
Pia Ngole alibainisha kuwa Serikali
imeongeza idadi ya wanaufaika wa mikopo kwa kuzingatia vipaumbele vinavyotokana
na mahitaji ya Taifa.
Ngole amebainisha kuwa mafanikio hayo
ni matokeo ya utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya awamu ya nne inayosema Hapa
Kazi tu.
Aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea
kufanya kazi kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano itakayowezesha kutoa
mikopo kwa wakati kwa kuzingatia sheria Kanuni. na Taratibu za utoaji mikopo.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya juu ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.9 ya mwaka
2004 na kuanza rasmi mwezi julai, 2005.ambapo Katika mwaka wa Masomo 2005/2006
idadi ya wanafunzi waliopata mikopo ilikuwa 42,749 ambapo jumla ya bilioni 56.1
zilitolewa.
Post a Comment