HIGHNESS KIWIA aondoa Kesi ya Kupinga Matokeo ya Ubunge wa ILEMELA Jijini Mwanza
Agrey Laban ambae ni Katibu wa Highness Kiwia akizungumza na Wanahabari nje ya Mahakama.
Na:George Binagi
Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza leo imetupilia mbali kesi ya Kupinga Matokeo ya ubunge
katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea
ubunge katika jimbo hilo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
Haighness Kiwia.
Katika kesi hiyo ambayo ni namba mbili ya mwaka
2015 iliyofunguliwa Novemba 25 mwaka jana, Kiwia alikuwa akipinga ushindi wa
mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula kupitia Chama cha Mapinduzi CCM
kutokana na madai ambayo ni pamoja na kuendesha kampeni za ubaguzi wa kikabila
sanjari na kupata kura ambazo hazikuendana na idadi ya wapiga kura
walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Kesi hiyo imefutwa baada ya Kiwia kupitia kwa
mwanasheria wake Paul Kipeja kuiomba Mahakama kufuta kesi hiyo kwa madai ya
kwamba mteja wake ameshindwa kulipia gharama za Mahakama ambazo ni Shilingi
Milioni 10 na kwamba washtakiwa walikuwa ni Angelina Mabula pamoja na
Mwanasheria wa Serikali ambapo gharama ya kufungua kesi hiyo kwa kila
mlalamikiwa ilikuwa ni shilingi Milioni Tano.
Kufuatia ombi hilo, Msajili wa Mahakama Kuu
Kanda ya Mwanza Eugenia Gerald Rujwauka alitoa maamuzi ya kuifuta kesi hiyo
kama ambavyo mlalamikaji alivyoomba.
Baada ya kesi hiyo kufutwa, Mutabanzi Julius
Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea mlalamikiwa,
amebainisha kuwa baada ya maamuzi hayo anatarajia kukutana na mteja wake ili
kujadiliana hatua za kuchukua na huenda akafungua kesi ya madai dhidi ya Kiwia
kutokana na kufungua kesi na kisha kuiondoa mwenyewe na hivyo kumuingiza mteja
wake katika gharama zisizo za lazima.
Ifahamike kwamba Angelina Mabula pamoja na Highness Kiwia hawakuhudhuria Mahakamani hapo na hakukuwa na wafuasi wengi wa vyama vya siasa kama ilivyozoeleka ambapo nje ya Mahakama hiyo, Agrey Laban ambae ni Katibu
wa Kiwia ameilalamikia Mahakama kutokana na kushindwa kupunguza gharama za kesi
hiyo jambo ambalo limepelekea haki kupotea.
Wakati hali ikiwa hivyo, Kheri James ambae ni
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula, amepongeza maamuzi ya kesi
hiyo kufutwa na kuongeza kuwa hatua hiyo inatoa wigo wa mbunge huyo kuwatumikia
wananchi.
Akiwa ofisini kwake, Katibu wa CCM Mkoa wa
Mwanza Miraji Mtaturu akapata fursa ya kuzungumzia Maamuzi ya Mahakama juu ya
kesi hiyo ambapo amempongeza Mabula kwa uvumilivu wake kwa kuwa kiongozi akiwa
na kesi Mahakamani anakosa uimara wa kuwatumikia wananchi.
Katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka
jana, Angelina Mabula (CCM) aliibuka mbunge wa Jimbo la Ilemela kwa kupata ushindi
wa kura 85,425 na hivyo kumshinda mpinzani wake wakaribu kutoka Chadema Highness
Kiwia aliekuwa akitetea jimbo hilo ambae alipata kura 61,679.
Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama.
Mutabanzi Julius Lugaziya ambae ni Mwanasheria Mwandamizi aliekuwa akimtetea Angelina Mabula akihojiwa na Wanahabari nje ya Mahakama.
Katibu wa Mbunge wa Ilemela Kheri James (mwenye miwani) akiwa katika mahojiano na wanahabari nje ya Mahakama.
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama.
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama.
WanaCCM wakieleza namna walivyopokea maamuzi ya Mahakama.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akieleza namna alivyopokea maamuzi ya Mahakama.
Post a Comment