Header Ads

Vivutio Vingine vya Utalii Vyaibuliwa Katika Hifadhi ya MKINGU, Morogoro

Hifadhi asili ya Mkingu ipo wilaya  ya Mvomero  Mkoani  Morogoro, Hifadhi hii ni eneo muhimu sana kiutalii kutokana na upekee wake wa maisha ya viumbe, mimea  pamoja na maisha ya binadamu kiujumla.

Hifadhi hii  ina ukubwa wa hekta 26, 334 na  imezungukwa na vijiji vitano ambavyo vipo ndani ya kata sita  na tarafa mbili.

Tangu kuanzishwa kwake Hifadhi hii   mwaka 2016,  Serikali  kupitia   Wizara ya Maliasili na Utalii  chini ya  Wakala wa Huduma ya  Misitu Tanzania ( TFS)  imekuwa ikihudumia  hifadhi  hii kutokana na kuwa na mimea na viumbe ambavyo ni vivutio pekee vya Utalii nchini ambavyo havipatikani mahali popote duniani.

Huyu ni aina mojawapo ya  chura ambaye hapatikani mahali popote duniani isipokuwa katika Hifadhi ya Mazingira asili ya Mkingu ambaye ni mojawapo ya kivutio cha utalii katika hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Mazingira asili ya Mkingu, Bw. Abeid Kindo anasema kutokana na sifa  hizo za kipekee zinazopatikana katika Hifadhi  hiyo  imekuwa na umuhimu wa  aina mbili ambao ni umuhimu wa kidunia na umuhimu wa   kitaifa, Katika umuhimu wa kidunia  upo  katika viumbe, mimea na wanyama.

Anasema hifadhi hii ina   wanyama wenye uti wa mgongo 392  kati ya hao 32 hawapatikana mahali   popote duniani isipokuwa ni  Mkingu tu yaani ni endemic species. Aidha , alisema kuna vyura na ndege wanaopatikana katika hifadhi hiyo tu.
Bw. Kindo anasema kuwa hifadhi  hiyo imejaliwa kuwa na   wanyama wanaotambaa 42 kati ya hao 14  hawapatikanimahali  popote duniani isipokuwa Mkingu tu pamoja na  aina ya ndege  214 kati ya hao ni aina nne ndio wanaopatikana katika hifadhi hiyo.

Mbali na hiyo, Amesema kuwa ndani ya hifadhi  kuna msitu unaotumika kwa masuala ya mila za Waluguru kuwa  eneo hilo ni zuri sana  amabalo nalo ni kivutio cha utalii ndani ya msitu huo
Maporomoko Lusingizo yenye mita zaidi ya 50 yaliyoko katika Hifadhi ya Mazingira Asili ya Mkingu  ambayo ni mojawapo ya kivutio cha Utalii katika Hifadhi hiyo,  Hadi hivi sasa kuna wawekezaji wamejitokeza ili waweze kuzalisha umeme katika kivutio hicho cha utalii.
 Mbali ya kupatikana kwa wanyama na mimea katika Hifadhi hiyo Bw, Kindo anaeleza kuwa kuna pango la Malolo  ambalo wenyeji wa Mkindo wana historia kubwa  ya pango  hilo ambalo wenyeji  hawataweza kusahau kwani kuna mwanaume mmoja  aliiba mke wa Mtu akaishi naye ndani ya pango hilo kwa muda wa miaka 3 bila kujulikana kijini. Pango hilo lina vyumba mithili ya nyumba iliyojengwa.

Pia anasema kuwa nadni ya hifadhi hiyo  kuna pango ambalo ukikaa nje kuna upepo unaotoka ndani unapuliza hiyo ni ishara tosha kuwa humo ndani ndani kuna uhai.

Anabainisha kuwa hifadhi hiyo  ina  jiwe lenye alama za nyayo za binadamu, kwato za mifugo ikiwa hiyo  ni ishara tosha kuwa  maisha ya kale ya binadamu yalianzia ndani ya hifadhi hiyo. 

Aliongeza kuwa mbali ya mapango  ndani ya hifadhi hiyo , kuna maporomoko Lusingizo yenye mita zaidi ya 50 ,  hadi hivi sasa kuna wawekezaji wamejitokeza ili waweze kuzalisha umeme katika kivuto hicho cha utalii.

Pia kuna magofu ya kale ya Wajerumani ambayo waliishi ndani ya hifadhi kabla vita vya pili vya dunia na baada ya kuondoka kwa Wajerumani  ilikuwa shule ya msingi ya  kijiji cha Mafuta, na baada ya eneo hilo likatangazwa kuwa hifadhi , Shule ile ilitolewa na kujengwa kijijini.

Bw. Kindo anasema licha ya hifadhi hiyo kuwa na vivutio lukuki bado  imekuwa ikitembelewa na idadi ya  watalii isiyoridhisha  licha kwa   mwaka jana wameweza kupata watalii 75 kutoka  Ujerumani.

‘’Tokea mwaka jana hadi hivi sasa tumeweza kuibua vivutio  saba vya utalii na  tunaendelea kufanya  jitihada za makusudi  ili kuhakikisha tunakuwa na vivutio vingi vya utalii ili tuweze kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi ‘’.alisema Bw. Kindo.

Aidha,Alisema  Hifadhi hiyo ndio chanzo cha mto Wami, mto  Ruvu na Mto Mkingu ambapo maji hayo yamekuwa yakitumika katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo,uvuvi,mazalia na makazi ya mimea na wanyama bila kusahau maji hayo ndiyo hutumika kuwanyesha wakazi wa Dare s Salaam na mikoa ya  jirani.

Amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali  wasisubili watafiti kutoka nje ya nchi kwenda kufanya tafiti katika Hifadhi hiyo badala yake wao wawe mstari wa mbele katika kuvumbua vitu vingi ambavyo vinapatikana katika hifadhi hiyo

Baadhi ya sehemu za kuvutia katika Hifadhi ya Mazingira Asili ya Mkingu ambayo ni njia  mojawapo inayotumiwa na watalii kwenda kijiji cha Maskati kuangalia vivutio vya Utalii vinavyopatikana katika Hifadhi hiyo. 

 ( Picha na  Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii)

No comments

Powered by Blogger.