Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa
Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe,( kushoto) akishuhudia
uchambuaji wa barua za maombi ya zabuni ya kununua madini ya Tanzanite wakati
wa mnada.
Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini wa Wizara
ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe alisema kuwa pamoja na manufaa
yaliopatikana katika mnada huo, Serikali itaendelea kuboresha mnada huo kwa
kuongeza muda zaidi ili kutoa fursa kwa kila
mfanyabiasha wa Tanzanite kushiriki; Vilevile kuwepo na majadiliano zaidi kati ya wauzaji
na wanunuzi wa madini ya Tanzanite ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Profesa Mdoe aliongeza kuwa lengo la Serikali katika
mnada huo ni kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite kupata matokeo chanya na yenye tija katika shughuli zao, pia Taifa linufaike
kutokana na matokeo hayo kwa njia mbalimbali.
Mmoja wa wafanyabiashara ya madini ya Tanzanite,
ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzaniteone Faisal Shuhbhai aliipongeza
Serikali kwa kuweka utaratibu huo ambao ni
wa kwanza kufanyika nchini kwakuwa utawawezesha wafanyabiashara hao
kufanya shughuli zao kwa ufanisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Faisal alisema kuwa utaratibu wa mnada
utawawezesha wafanyabiashara wa Tanzanite waliokuwa wakikwepa kodi, kulipa
mirabaha kwa wakati baada ya kuwepo kwa mpango huo ambao haukuwepo hapo awali;
Aidha utawasaidia wafanyabiara kupata bei elekezi inayoendana na soko la dunia
na hivyo kuacha kutorosha madini ya
Tanzanite nje ya Tanzania kwa madai ya kutafuta masoko.
|
Post a Comment