Wizara ya Habari yapokea Ipad kwa Ajili ya Maafisa Habari wa Mikoa 13
Na Dotto Mwaibale
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye amepokea Mini Pads za kisasa 180 zenye thamani takribani milioni 90 kutoka kwa kampuni StarTimes Tanzania kwa ajili ya kuwarahisishia kazi wafanyakazi wa wizara yake.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo ndani ya jingo la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Dar es Salaam, Mh. Nnauye amebainisha kuwa Mini Pads hizo zitarahisisha kwa kiasi kikubwa wafanyakazi wa wizara yake kuendana na kasi ya ukuaji wa TEHAMA katika kufanya shughuli zao hususani tafiti.
“Wizara yetu inashughulika na Sekta Nne Kubwa. Nazo ni; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Sekta hizi ndizo zinazokamilisha jina la Wizara yetu. Wizara yangu inashirikiana na Wizara, Taasisi na wadau mbalimbali katika kuletea maendeleo wahusika katika sekta tajwa. Katika Nchi yetu tunazo Halmashauri zaidi ya 170 ambazo kimsingi kila Halmashauri inapaswa kuwa na Ofisa mmoja kwenye kila sekta zetu, hivyo maafisa 4 kwa ajili ya sekta Nne.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape
Nnauye (wa pili kulia) akipokea moja ya Mini Pads 180 kutoka kwa Ofisa Mtendaji
Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (wa kwanza kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kurahisisha
ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Wakishuhudia tukio hilo wa pili
kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing
na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel (kulia).
Waziri
wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akifurahia
kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha
ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu
Mkuu wa wizara hiyo, Profesa, Elisante Ole Gabriel na wa pili kushoto ni Balozi wa
Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu
Youqing na muwakilishi kutoka ubalozini Bw. Mr Gao Wei.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye (wa pili kushoto), akiteta jambo baada ya kupokea Mini Pads 180 kutoka
kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi
wa wizara hiyo. Pamoja naye kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes
Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel
na kushoto ni Balozi wa Jamhuri
ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dr. Lu Youqing.
.............................
Kimuundo tunakuwa na Afisa mmoja wa kila sekta kwenye kila Mkoa hivyo maafisa 4
kwenye kila Mkoa wa ngazi ya Mkoa.” Alisema Mh. Nnauye
“Baada ya kutafakari kwa kina, tukaona tuanze na kuboresha
mawasiliano kwa maafisa wetu ndani ya Wizara, Baadhi ya Mikoa na pia
Halmashauri. Tunaamini kwamba mawasiliano madhubuti yakiwepo, itakuwa rahisi
kufanya ufuatiliaji wa kina na kuboresha utendaji.
Kwa kutambua kwamba kuna haja ya kushirikisha wadau mbali mbali tuliwasiliana pia na kampuni ya Star Times ambayo ni mbia wa TBC kwa ajili ya kutusaidia wanaloweza kwa ajili ya kuanza uboreshaji wa vitendea kazi vya mawasiliano katika sekta zetu.” Aliongezea

“Ni faraja kubwa kuona kwamba
wenzetu wa Sar Times wametuelewa haraka na kukubali kutusaidia vifaa hivi vya
mawasiliano (Mini Pads) zipatazo 180.
Kwa hakika vitatusaidia sana kuboresha utendaji kimawasiliano kwa maafisa wetu wa Wizara na pia Maafisa mawasiliano ambao ni wadau wa kutoa taarifa kwa umma,” alisema na kuhitimisha Mheshimiwa Nnauye, “Ifahamike kwamba kwa jinsi dunia inavyobadilika kwa kasi kubwa sana, masuala ya mawasiliano sio hiari tena bali ni lazima kuwa na mawasiliano ya kimkakati.

Mpango wetu ni kwamba maafisa wote ambao wanafanya kazi kwneye
Halmashauri zote, wapate mawasiliano japo hatua kwa hatua kwenye sekta zote
Nne. Tunawashukuru sana kampuni ya Star Times kwa msaada huu mzuri wa kuanzia.”
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji
Mkuu wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao alisema kuwa imekuwa ni
fursa kubwa kwa kampuni kuweza kufanikisha watanzania wanatumia vifaa
vinavyoendana na kasi ya maendeleo ya tekinolojia duniani kurahisisha kazi.
“Naweza kusema ni fursa ya kipekee
kwa Mheshimiwa Waziri kutuona sisi StarTimes kuwa tungeweza kuwatatulia
changamoto waliyokuwa nayo kwani zipo kampuni na taasisi nyingi ambazo
zingeweza kufanya hivyo. Hili naweza kusema limechangiwa kwa kiasi kikubwa na
jitihada tulizonazo katika kuwatumikia watanzania kwa kuwapatia huduma bora na
nafuu za matangazo ya dijitali.
Kwa kiasi kikubwa shughuli zetu tunazozifanya
huwezi kuzitenganisha na maendeleo ya tekinolojia ya habari na mawasiliano.
Ninaamini kupitia Mini Pads tulizozikadhi leo wafanyakazi wa wizara watakuwa na
fursa ya kupata huduma zetu bila ya wasiwasi wowote.” Alifafanua Bw. Liao
“Idadi ya Mini Pads tulizozikabidhi
hii leo ni 180 na tuna matumaini zitakuwa ni msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa
wizara kwa idadi iliyotajwa na mheshimiwa waziri. StarTimes tumejizatiti vya
kutosha si tu kuwahudumia wateja wetu bali pia kusaidiana nao katika shughuli
mbalimbali.
Kwa sasa kampuni yetu imelenga zaidi katika kuwekeza na kukuza vipindi na chaneli za nyumbani ili kuwapa watanzania wenye vipaji kuweza kuonekana. Tunashukuru sana ushirikiano tunaoupata kutoka serikali kwani ndio mdau mkubwa katika shughuli za uendeshaji wetu ambao ni zaidi ya miaka mitano sasa tangu tuanze.” Alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania.

Post a Comment