Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Serikali
imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee
kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.
Mpango
huo umetolewa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa wazee wa mkoa
wa Dar es Salaam alipokutana nao leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. amesema wazee wanakumbwa
na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema kuwa azma ya
Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao muhimu
ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika
vyombo vya maamuzi.
|
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na wazee wa mkoa wa Dare s Salaam
walipokutana katika kikao ofisini kwake Leo (Katikati) ni Mwenyekiti wa baraza
la wazee Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali na kulia ni katibu wa wazee hao Mohamed Mtulia.
|
|
Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali
akizungumza katika kikao cha wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto).
|
|
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu(Kulia) akionesha kitabu cha sera ya wazee ambayo inatarajiwa
kuandikiwa mswaada wa kuwa sheria na kupelekwa Bungeni kushoto ni Katibu Mkuu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
.................................
|
“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa
kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bunge mwezi Septemba
ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza
masuala yahusio wazee” Alisema Mhe.Ummy.
Naye
mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada
katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt
John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara
ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na Waziri
husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania waishi katika
maisha mazuri.
Aidha
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao
kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa
wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee
kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika
maeneo mengi zaidi.
Kikao
hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na
Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kujadili mshtakabali wa maendeleo ya
wazee nchini.
Post a Comment