Vijana Waandaa Msafara wa Hisani Kupinga Vitendo vya Ujangili na Kuhamasisha Utalii wa Ndani
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia maelezo ya wawakilishi wa Bongo ride charity cruise kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani
......................
|
Vijana wa Bongo Ride, kwa ushirikiano wa vijana wenzao wa Team Tezza na TanzaniaZalendo wanayo furaha kuwatangazia umma wa watanzania kukamilika kwa maandalizi ya msafara(cruise) wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,
Ujangili hapa nchini kwa miaka ya hivi karibuni umeongezeka ikiwa ni matokeo ya mahitaji makubwa ya pembe za ndovu,pembe za kifaru na pia ngozi ya chui na bidhaa mbalimbali za wanyamapori.
Hivi sasa biashara ya wanyamapori na rasiliamali za asili imeshika nafasi ya nne kwa biashara haramu inayowafaidisha wengi duniani,baada ya madawa ya kulevya ,silaha na usafirishaji wa binadamu inakadiliwa kuwa na thamani ya dola zaidi ya 284 billion za kimarekani.
Hali hii inatisha licha ya kuwaeimisha vijana kuwa wanaweza kuwa mabalozi wa kulinda wanyamapori pamoja na rasilimali za nchi yao,pia wanatakiwa kutuma ujumbe watu waweze kuchukua hatua kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa amesema “ tumezindua awamu ya tatu ya Bongo Ride Charity Cruise ikiwa ni matokeo ya kuweza kusaidia jamii.Tukiwa na washiriki zaidi ya mia 2 wa hapa nchini na zaidi ya washiriki elfu 2 Afrika mashariki. Katika awamu yetu ya kwanza tulifanya msafara wa hisani kusaidia wagonjwa waliopata ajali katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani kwa kuwapatia mashuka yakutandika pamoja na kujifunikia na pia Mwaka jana tuliweza kwenda Mkoani Morogoro na kusaidia watu waishio na virusi vya UKIMWI Morogogo (WAVUMO) ikiwa nia ni kuhamasisha amani na upendo katika nchi yetu na awamu hii tumeamua kufanya ”YOUTH AGAIST POACHING” ili kufikisha ujumbe kwa vijana wenzetu na serikali kwamba tnapinga ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani kama wazalendo na wapenda maendeleo.
“Malengo yetu ni kuwa na tukio la kihistoria tukiwa na nia ya kumfanya kijana wa Kitanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio vilivyomo ndani ya nchi pamoja na kuwa balozi mzuri na mzalendo wa Nchi yake” Aliongeza Magesa
Mkuu wa matukio wa Bongo Ride Kelvin Edes akiongea alisema Tunategemea kuwa na siku tatu za mbio hizi za hisani za magari kuanzia Dar es salaam kuelekea Arusha tukiwa na washiriki zaidi ya mia 200 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Pia tutakuwa na muda wa kuongea na vyombo vya habari, kutembelea shule na kuzunguka katikati ya mji kuweza kuongeza uelewa juu ya janga la ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.
“Siku ya pili tarehe 26 tutaungana na washiriki mbalimbali wa Arusha na tutaelekea Hifadhi ya wanyama Tarangire na kujionea mambo mazuri ya hifadhi hiyo na kujifunza zaidi. Jambo hili litasaidia zaidi watu kuwapa hamasa ya kwenda kujionea vivutio vya hifadhi za ndani na kumfanya kijana ajionee utajiri uliomo ndani ya nchi yake.
Tunaamini kabisa kasi ya kuuliwa kwa maalbino imepungua kwasababu wao wenyewe wanaweza kuzitetea nafsi zao, lakini Tembo, Kifaru na wanyama wengine wanaokumbwa na janga la ujangili hawawezi kuzitetea nafsi zao na kuomba msaada, Hivyo sisi kama vijana tumejitolea kuwa mstari wa mbele kupaza sauti zetu na kutetea haki zao kwani nao wanastahili kuishi, ”Aliongeza
Meneja Mawasiliano wa Bongo Ride Krantz Mwantepele alinukukuliwa akisema kuwa vijana wakipaza sauti zao itaamsha matumaini kuwa imefika wakati kuwa ujangili ni jambo linalotakiwa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukomeshwa .
“Sisi kama vijana tunaumizwa na kuongezeka kwa matukio haya ya ujangili ,uhujumu wa rasilimali ni matukio yote yanayopangwa na watu wenye tamaa za mafanikio ya haraka na kutamalaki kwa rushwa miongoni kwa viongozi na wanajamii.”
Pia Mkurungezi na mwanzilishi wa Team Tezza Kenan Richard aliongeza kuwa vijana wanataka sauti zao zisikilizwe, kwa maana hawataki kuwa kizazi kitakachowasimulia wajukuu zao kuwa hawakufanya jambo lolote juu ya haya na wanaomba vijana wenzetu na viongozi wa dunia kuungana nasi ili kupinga biashara haramu ya ujangili.
KUHUSU BONGORIDE CHARITY CRUISE;
Bongo Ride Charity Cruise ilianzishwa mwaka 2014 ikiwa na lengo la kuisaidia serikali na jamii kiujumla kutatua baadhi ya matatizo yanayoizunguka jamii ya Kitanzania na Afrika kwaujumla kwa njia ya kupaza sauti kuhusu jambo lolote linaloonekana kuwa tatizo kwa namna tofauti.
Nia yetu ni kuzunguka mikoa yote Tanzania na Afrika kwa kutumia njia ya kusafiri kwa pamoja na magari yetu binafsi na kutoa misaada sehemu mbalimbali katika bara letu la Afrika, Pia kumfanya kijana wa Kitanzania kujifunza tamaduni mbalimbali na kukuza wigo wa marafiki wenye msaada kwake ili kuongeza sababu lukuki za kimaendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla.
KWA MAELEZO ZAIDI; WASILIANA NA
KRANTZ MWANTEPELE
MENEJA MAWASILIANO BONGORIDE
NAMBA YA SIMU;0712579102
EMAIL;krantzcharles@gmail.com
Post a Comment