Milipuko yatokea Mjini BRUSSELS watu Kadhaa Wafariki Dunia
Moshi umeonekana ukitanda angani kutoka kwa moja ya majengo katika uwanja huo.
Serikali ya Ubelgiji imethibitisha kwamba kunao watu waliojeruhiwa lakini haijasema idadi.
Watu wameondolewa kutoka kwenye uwanja huo na safari za ndege kutua au kupaa kutoka uwanja huo kukatizwa.
Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba kuna watu wamejeruhiwa katika ukumbi wa kuhudumia watu wa safari za kuondoka nchini na kwamba milipuko ilitokea karibu na meza ya shirika la ndege la American Airlines.
Milipuko pia imeripotiwa katika kituo cha treni cha Maelbeek karibu na majengo taasisi za Umoja wa Ulaya.
Mfumo wa uchukuzi wa treni mjini Brussels umefungwa.
Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.
Haijabainika ni nini chanzo cha milipuko hiyo.
Post a Comment