Serikali yapongeza Juhudi za Chuo cha AGA KHAN katika Sekta ya Afya Nchini
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imebainisha kuwa itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi katika kuleta maendeleo kwenye nyanja mbalimbali hapa nchini huku ikipongeza juhudi zinazofanywa na Taasisi ya mtandao ya Agha Khan kwa jitihada zake kufundisha wataalam wa sekta ya Afya.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 31.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga katika ngazi ya digrii katika chuo cha Agha Khan, Jijini Dar es Salaam.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Chuo hicho Kikuu cha Agha Khan kwa kuanzisha shule hiyo wanaongeza idadi ya vyuo vitakavyokuwa vikizalisha kwa wingi wataalam watakaokuwa wakipta digrii kwani awali kulikuwa na upungufu mkubwa.
Jengo la Chuo hicho cha Uuguzi na Ukunga, limefanyiwa ukarabati pamoja na kupatiwa vifaa mbalimbali kwa msaada wa Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo waliwezesha kwa kugharamia ujenzi wa jengo hilo pamoja na vifaa vya kisasa vya kufundishia.
Kwa upande wake, mgeni rasmi mwakilishi wa Serikali ya Ujerumani, Waziri wa Uchumi na Maendeleo, Dk. Gerd Muller ambaye alibainisha kuwa, wanataka kuona watalaama wengi wa sekta ya afya wanapata elimu ilikuondokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili wanadamu na kuongeza kuwa, bila wataalam wa tiba, Jamii haitakuwa salama.
Aidha, katika tukio hilo,wageni na viongozi mbalimbali walipata kulitembelea jengo hilo pamoja na kushuhudia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea shuleni hapo.
Tazama tukio hilo hapa:
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahia jambo na Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller na wageni mbalimbali waliojumuika katika tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la shule ya Uuguzi na Ukunga ngazi ya digrii katika Chuo Kikuu cha Agha Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi na watumishi wa Chuo hicho wakiwa katika tukio hilo.
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akisisitiza jambo..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo..
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akitoa maelezo mafupi kabla ya kuzindua rasmi jengo hilo la shule ya wauguzi na wakunga katika chuo kikuu cha Agha Khan..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba ya Serikali namna Wizara Afya itakavyonufaika na wataalam wa sekta ya Afya watakaopata elimu katika shule hiyo.
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akifungua rasmi jengo hilo.
Wageni mbalimbali wakifuatilia tukio hilo.
Msimamizi wa shule hiyo ya Uuguzi na Ukunga akitoa maelezo machache kwa wageni mbalimbali..
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi huo..
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akiangalia namna ya vifaa vya kisasa vya kufundishia jinsi viavyotumika wakati wa kutoa huduma Hospitalini.
Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller akijaaribu kupata vipimo kuashiria ufunguzi wa jengo hilo pamoja vifaa vya kisasa vilivyowezeshwa na Serikali ya Ujerumani. Kushoto kwake ni Dk. Kigwangalla akimwelezea jambo la kitaalam juu ya vipimo hivyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari namna Serikali itakavyonufaika kupitia shule hiyo.
Post a Comment