Ubunifu wa Mavazi Jijini Mwanza Wapata Ufumbuzi
Idda Hassan ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushonaji wa Mavazi Jijini Mwanza ya Mikaela Professional Tailors akionyesha moja ya mavazi yanayoshonwa na Kampuni hiyo.
Na:George Binagi
Tofauti na ilivyo katika majiji mengine kama vile Jijini Dar es salaam, Jiji la Mwanza halina mwamko mkubwa katika ubunifu wa mavazi.
Ni kutokana na hali hiyo, Wataalamu na Mabingwa wa Ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali (Kike na Kiume) Jijini Mwanza, Mikalela Professional Tailors, wameahidi kulitambulisha Jiji hilo katika ubunifu wa mavazi ili kuendana na kasi iliyopo katika majiji mengine.
"Awali nilikuwa nateseka sana. Nguo zangu nilikuwa nikishea Jijini Dar au Arusha na nikizivaa watu wengi wakawa wanauliza niliposhonea na kutamani niwapeleke. Nikaona kumbe Mwanza kuna uhitaji mkubwa wa ubunifu na ushonaji wa mavazi hivyo nikaamua kuanzisha kampuni ya ubunifu na ushonaji wa mavazi ya Mikaela Professional Tailor ili kukata kiu hiyo. Alisema Idda Hassan ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo.
Post a Comment