..................
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika wa Usuluhishi wa Mgogoro
wa Libya, amewasili jana Jijini Tunis nchini Tunisia kushiriki Mkutano wa
8 wa Nchi majirani wa Libya.
Mkutano huo umeitishwa na Serikali ya
Tunisia, na ni muendelezo wa jitihada za nchi majirani kusaidia kuleta hali ya
amani na usalama nchini Libya.
Rais Mstaafu Kikwete amewasili Tunis
akitokea Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la
Kuandika Katiba ya Libya.
|
Rais Mstaafu wa awamu ya nne na
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, akimkaribisha Waziri wa Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria
Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea hotelini
kwake katika Jiji la Tunis, Nchini Tunisia.
|
|
Rais Mstaafu wa awamu ya nne na
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, akiagana na Waziri wa Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria
Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea
hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini Tunisia.
|
|
Rais Mstaafu wa awamu ya nne na
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, akizungumza na Waziri wa Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa
Aljeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea
hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini Tunisia.
.................................
Katika mazungumzo hayo, Waziri
Messaleh amempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa Nchi
wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya.
Amemueleza hali ya
usalama na kisiasa ya Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya
namna bora ya utatuzi wa mgogoro huo, na akamhakikishia ushirikiano wa Serikali
ya Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa Afrika.
Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete
amemshukuru Waziri Abdelkader Messaleh kwa maelezo yake na ushirikiano
aliomuahidi na akamueleza matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro
huo hasa ikizingatiwa kuwa nchi jirani na Libya na Umoja wa Afrika
zitashirikiana na wadau wote kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa.
Rais Mstaafu Kikwete amesisitiza kuwa
suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya
wenyewe.
|
Post a Comment