Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea leo jijini Dar es
Salaam.Katika mkutano huo wachezaji walihakikishiwa kupokea ahadi yao kama
walivyo ahaidi kwa kuwa wamefanikiwa kuifunga timu ya Taifa wanawake Zimbabwe
licha ya kutoibuka na ushindi.
Picha na Frank Shija, WHUSM
Serikali kupitia
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetimiza ahadi yake ya kuwapa
motisha wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” kwa
kuwapa kila mmoja shilingi Laki tatu taslimu kutokana na kufanikiwa kutikisa
nyavu za Zimbabwe licha kutoibuka na ushindi.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia
James Wambura wakati wa mkutano wake na wachezaji hao leo jijini Dar es Salaam.
Wambura alisema
pamoja na Twiga Stars kufungwa kwa magoli 2-1 bado mmejitahidi sana katika
ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwenye mashindano kama hayo walikuwa
wanafungwa hadi magoli matano kwa sifuri.
Aliongeza kuwa
kutokana na jitihada hizo anatimiza ahadi yake ya kumpatia kila mchezaji kiasi
cha shilingi 300,000/= fedha ambazo anaamini zitawazidishia hari na morali ya
ushindi katika mchezo wa marudiano.
“Kutoka na na
jitihada zenu mlizozionyesha wakati wa mchezo huo ninatoa kwa kila mchezaji
kiasi cha shilingi 300,000/= na ahadi
hii inaendelea tena katika mchezo wa marudiiano” Alisema Naibu Waziri.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) Amina Karuma alitoa wito kwa wachezaji kuhakikisha katika
mechi ya marudio wanashinda kwa hari na mali ili kuonyesha thamani umuhimu wao
Aidha alitumia
fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuendelea kujitokeza kusaidia maendeleo ya
michezo hasa Soka la wanawake kwani kumekuwa na changamoto ya wafadhili hali
inayopelekea kusuasua.
Motisha hiyo kwa
wachezaji imetokana na michango ya wadau mbalimbali awalioguswa na timu hiyo
wadau waliochangia mpaka sasa ni TCRA (10,000,000/=), ASAS(2,000,000/=),
Mohamed Enterprises (2,000,000/=) na mdau ambaye akupenda jina lake litajwe
(3,000,000/=) na kufanya mpaka sasa kuwa na jumla ya shilingi milioni 17. Kwa
wadau wanaopenda kuchangia watumie Akaunti namba 20110001677 Twiga Stars Special Fund NMB Bank House, kwa
wale wanaotaka kuchangia vifaa waiwasilishe Wizarani mtaa wa Ohio Jengo la
Golden Jubilee Ghorofa ya nane.
|
Post a Comment