Wachezaji wa Mpira wa Magongo Watakiwa Kujituma ili Kuiletea Sifa nchi.
Na.
Najaha Bakari
Wachezaji wa
mpira wa Magongo (Twende Hockey) wametakiwa kujituma na kuiletea sifa nchi katika mashindano yao ya
kufuzu kombe la Afrika yanayotarajia kufanyika
Machi 18 hadi 28 mwaka huu nchini Namibia.
Rai hiyo
imetolewa na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
wakati wa kukabidhibendera kwa timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
“Nawatakia
mafanikio katika mashindano hayo, muwe na moyo wa kushinda siyo kushiriki, na
nawaahidi kuwapokea mkirudi na ushindi“alisema Mhe. Nnauye”.
Aidha, Mhe.
Nnauye amesema kuwa Serikali itakuwa karibu na Vyama/Mashirikisho ya michezo
ili kuhakikisha kuwa michezo yote inafanya vizuri kwa lengo la kuitangaza na kuiletea sifa nchi
yetu.
Waziri Nnauye
aliwaomba NMB na wadhamini wengine
kusaini mikataba ya muda mrefu kwani matokeo mazuri hupatikana kwa kuwekeza kwa
muda, vilevile aliwataka wadhamini
kudhamini michezo yote na siyo soka pekee.
Kwa upande
wake Afisa fedha Mkuu kutoka NMB Bw. Waziri Barnabas alisema kuwa NMB imekuwa ikidhamini
mchezo huo kwa miaka miwili sasa na michezo mingine,ambapo aliwataka wanamichezo kuwa na ari ya kuleta
ushindi na sifa kwa Taifa kuwafanya
wadhamini kuwa na moyo wa kudhamini zaidi.
Awali
Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo Bw. Abraham Sykes, alisema
mchezo huo ulisahaulika ila anaamini kuwa vijana wake wameandaliwa vyema hivyo
watafanya na wataendelea kufanya vizuri.
Timu ya Mpira
wa Magongo inatarajia kuondoka nchini tarehe 13 Machi mwaka huu kuelekea nchini
Namibia kwa mashindano hayo, ambapo NMB wamewakabidhi hundi ya Sh.milioni 25 na
mabegi ya kuweka vifaa vya mchezo huo.
Post a Comment