Uchanguzi wa Marudio Unaendelea Visiwani ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dr Ali Mohamed Shein wa tatu toka mbele akiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura katika kituo cha Kibere.
Makamu Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassani akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha kiembe samaki mjini Unguja.
Masanduku ya kura.
Mawakala wa vyama mbali mbali wakiwa ndani ya chumba cha kura kwa ajili ya kazi.
Bibi akisindikizwa kwenda kupiga kura katika kituo cha Mwembeladu.
hali ya usalama nayo iko vizuri.....
Babu akiwa tayari kwa kupiga kura,utaratibu maalum umewekwa kwa wazee wetu.
Vijana wa jang'ombe wakiwa tayari wameshapiga kura.
Wananchi wakipiga kura katika kituo cha Skuli ya Mwembeladu.
Baadhi ya wananchi wakihakiki majina yao kabla ya kuingia kupiga kura katika kituo cha skuli ya Raha Leo.
....................
Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia
Suluhu Hassani amepiga kura katika kitua
cha kiembe samaki mjini Unguja.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura amesema kuwa
amefurahishwa na mwitikio kutoka kwa wananchi na kuwaomba wananchi ambao bado
hawajapiga kura kufanya hivyo.
Aidha Bi Samia amesema kuwa hali ya Usalama ni shwari na
kuwatoa hofu wananchi kwani usalama upo wa na uwakika,”wananchi wasiwe na hofu
usalama upon a hakuna vurungu zozote na wasii ambao bado hawapiga kura watoke
kupiga kura”Samia
Aidha katika baadhi ya vituo nilivyopata kutembelea asubuhi
hii wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa
imeimarishwa.
katika kituo cha shule yasekondari Muembeladu ambayo ina vituo
sita na vituo vitano vinawatu 350 na kituo kimoja kina watu 91 akizungumza
msimamizi wa kituo hicho amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri
katika jimbo la Jangombe .
kwa upande wa kituo cha skul ya Muembeshauri nako hali ni
shwari na zoezi linaendelea vizuri ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika
watu kupiga kura, zoezi hilo limeanza vizuri kwa katika eneo hilo la Muembe
shauri ambapo ni Jimbo la Raha Leo.
Zoezi katika Jimbo la kikwajuni linaendelea vizuri huku
mwitikio wa watu ukiwa ni mkubwa waliojitokeza kupiga kura ambapo katika kituo
cha skul ya Raha Leo.
Wakizungumza baadhi ya wananchi walijitokeza kupiga kura
wamesema zoezi hilo limekua rahisi na amani tofauti na taarifa zilivyokua
zinsambazwa katika mitandao.
Mkazi wa Muembeshauri aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu
Salum Haji ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwani zoezi la kupiga
kura linaendelea kwa amani na utulivu.
Aidha ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kusimama imara na wa
moja katika kipindiki ambapo watu wasio takia mema Zanzibar wakijitahidi kutaka
kuwagawa wazanzibar kwa misingi ya ikikadi za kisiasa.
“ndugu zangu tusikubali kugombanishwa na watu ambao wahaitakii
mema Zanzibar tusimame pamoja katika kutetea nchi yetu”amesema Haji
Wakati zoezi hilo linaendelea maduka mengi yamefunguliwa na
wafanya biashara wakiendelea na kazi kama kawaida,kwa upande wake
mfanyabiashara Musa Jackson amesema zoezi limekua safi na kuomba wananchi
wajitokeze.
Amesema kuwa ni vyema watu wajitokeze kuchangua viongozi na
kuacha kususia uchanguzi huo,”wananchi wajitokeze waache kususa kwani haisadii
na kufanya hivyo ni kupoteza haki yako”amesema
katika jimbo la Mpandae zoezi linakwenda vizuri kwa wakinamama
wengi kujitokeza katika skul ya Jangombe.
Post a Comment