Header Ads

Kilimo chamkomboa Mama Mjane Mwenye Ulemavu wa Miguu, BUMBULI wilayani LUSHOTO

 Bi. Zaharia Ally (54) akiwa na wajukuu zake nyumbani kwake.

Bi. Zaharia Ally ambaye hayupo pichani hutembea umbali wa Kilometa zaidi ya Tatu  kutoka kwake kufika katika eneo hili  kufuata kuni kwa Mahitaji ya Nyumbani ikiwemo kupikia.

Eneo hili ni Shamba la Bi. Zaharia Ally kwa ajili ya Kilimo cha Maharagwe na Mahindi.


Hapa ni Nje ya nyumba ya Bi. Zaharia (Ambaye hayupo pichani) akionesha mzigo wa kuni.


 Na Blogs za Mikoa Tanzania.

kuna haya maneno yanasema kuwa Ardhi ni moyo wa mwanamke katika kujikomboa kimaisha

Pamoja na jitihada mbalimbali za kumwendeleza mwanamke katika kujikwamua na umaskini raslimali ya ardhi ndiyo chachu kubwa ya kuwawezesha wanawake kujikwamua na umaskini hapa nchini.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 54 anaetambulika kwa jina la Zaharia Ally mkazi wa Bumbuli wilayani Lushoto, mkoani Tanga ni miongoni mwa wanawake wanye changamoto za maisha na wanaopambana kujenga familia zao.

Mwanamke huyo ambaye ni mjane na mlemavu wa mguu amekuwa akijikita katika kilimo jambo linalomuwezesha kuweza kujikimu kimaisha na familia yake yenye watoto wanne.

Ingawa mwanamke huyo ni mjane kwa zaidi ya miaka 15 kilimo kimekuwa mkombozi mkubwa kwake baada ya na kuonyesha ukomavu kwamba mwanamke akitambua wajibu wake katika familia hata akipatwa na matatizo anapambana kuhakikisha anamudu majukumu yake kama mama katika familia.

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania wananchi wanaojihusisha na kilimo na ufugaji ni zaidi ya asilimia 70% ambapo wanawake ndiyo chachu ya maendeleo katika kazi zote hizo.

Wanawake wanaadhimisha siku yao tarehe 08.03 2016 ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu inasema '50 kwa 50 ifikapo 2030 tuongeze jitihada'.

Siku hii huwa ni mahsusi kwa wanawake kukutana katika maeneo mbalimbali na kukumbushana mambo muhimu katika kuondokana na mfumo dume katika jamii na kupiga hatua za maendeleo.

Hata hivyo taasisi binafsi pia zitajumuika katika siku hiyo ambapo Oxfam Tanzania kupitia mradi wake wa  Grow unaoendesha shindano la mama shujaa Wa chakula watakua mkoani Mtwara kushererekea na kutoa ujumbe kwa jamii hasa umiliki Wa ardhi kwa wanawake

No comments

Powered by Blogger.