Zoezi la Kuwapokea Wakimbizi Kutoka BURUNDI, Limeendelea Kambi ya Nyarugusu Mkoani KIGOMA
Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya
Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile
akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambiza
Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini
Burundi hivikaribuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya
Nyarugusu.
Wakimbizi kutoka nchini Burundi
wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani
Kigoma ambapo wamehifadhi wa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi
za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa na Wizaraya
Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa
la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya kimataifa ili
kuwapatia makazi salama.
Mtoto Jamine Nibetanga (14),
kutoka nchini Burundi akiandaa chakula katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi
kutoka nchini Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye
kambizaNduta, KaragonaMtendeli.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi,
KukimanaDafroza (katikati), akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi
ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma
ambapo wakimbizi kutoka Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya
kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni Mkabanura Eviline
(kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini
Burundi wakichota maji jana katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa
katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani
Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda. Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi
ina mpango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago, Mtendelina Nduta ili
kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi,
Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika
kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko
katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Shirika
la Red Cross ni mojawapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa
huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi Joseph Mtagura aliyeko
katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo yakuwauzia
wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi,
Ntirampeba Acquelina akianika mihogo ambayo huwauzia wenzake katika
kambi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Ugali wa
mihogo ni mojawapo ya vyakula muhimu vinavyotumika katikakambi ya
Nyarugusu.
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini
Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira
Wakimbizi hao wamekua wakiingia nchini kutokana na machafuko ya kisiasa
yaliyotokea nchini Burundi hivi karibuni.
Wakimbizi kutoka Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu.
Mkimbizi Haverimana Ejide
(kushoto) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula
cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa
maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya
Nyarugusu.
(PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
Post a Comment