Mkutano wa Bara la Afrika kujadili Mipango Endelevu na Mafunzo Kwa Vijana wafanyika, Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco toka Ubeligiji, Filip Lammens (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano wa kujadili Uwezeshaji kwa vijana ulioandaliwa na Don Bosco Kanda ya Afrika Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Don Bosco, Afrika Mashariki, Padri Eric Mairura (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu mkutano huo.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango na Maendeleo Afrika Magharibi wa Don Bosco, Tsedi Yao Ati akizungumza na wanahabari.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango na Maendeleo na Msimamizi wa Fedha na Uchumi wa Nchi za Maziwa Makuu, Rwanda, Burundi na Uganda, Br. John Njuguna akizungumza na wanahabari kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Don Bosco.
Mtunza Mitaala wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Rehema Binamungu (kushoto), akitoa mada katika Mkutano huo wa kujadili Uwezeshaji kwa vijana ulioandaliwa na Don Bosco Kanda ya Afrika Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwezeshaji akitoa mada.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Taswira katika chumba cha mkutano...
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo...
Na Dotto Mwaibale
CHUO cha Ufundi Stadi (VETA), kimesema kipo katika mchakato wa kuandika vitabu vya ufundi ili kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia nchini.
Hayo yalibainishwa na Mtunza Mitaala wa VETA, Rehema Binamungu katika Mkutano wa kujadili Uwezeshaji kwa vijana ulioandaliwa na Don Bosco Kanda ya Afrika Dar es Salaam leo.
Alisema vitabu hivyo vitasaidia kutoa elimu ya ufundi katika vyuo vingine na shule mbalimbali nchini.
Katika hatua nyingine Binamungu alisema Veta inahitaji kuwa na vifaa vya ufundi vya kisasa ili kukabiliana na kukua kwa teknolojia ya ufundi ambayo inahitaji kuwa na vifaa hivyo ili kwenda sambamba na soko la ajira.
"Kutokana na kukua kwa teknolojia kwa sasa tunahitaji vifaa vya kisasa na maboresho ya vifaa ili twende sambamba na soko la ajira,"alisema Rehema.
Aliongeza changamoto nyingine inatokana na chuo hicho kutoa elimu ya ufundi kwa watu wenye elimu tofauti hivyo jitihada zinahitajika ili kutoa elimu bora,"alisema Rehema.
Pia alisema VETA ipo katika mchakato wa kuandika vitabu vya kiufundi ambavyo vitasaidia kuinua elimu ya ufundi nchini.
Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana wanaopata mafunzo kwenye vyuo mbalimbali alisema ushirikiano unahitajika kati ya serikali na wadau mbali ili kuhakikisha wanashirikiana kutoa elimu bora na yenye manufaa kwa jamii.
Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Don Bosco Afrika Mashariki, Padri Erick Mairura alisema mkutano huo utasaidia kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini.
Alisema hali ya kiuchumi kwa vijana bado ipo chini hivyo ni vyema serikali na wadau wa elimu ya ufundi wakashirikiana kuandaa maisha bora kwa vijana.
Alisema mkutano huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini na utachangia kukuza ushirikiano kati ya sekta binafsi, wamiliki wa vyuo vya ufundi pamoja na serikali.
“Masomo ya ufundi yakitolewa ipasavyo yatasaidia kuwakwamua vijana katika changamoto mbalimbali hivyo ni muhimu sote tuone namna ya kuboresha vyuo vyetu na kuwawezesha vijana,” alisema Mairura.
Alisema anatoa wito kwa serikali kuviwezesha vyuo vya ufundi kwa kushirikiana navyo kwa karibu kama ambavyo nchi nyingine zinafanya.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Ofsi ya Mipango na Maendeleo Afrika Magharibi- Don Bosco, Tsedi Yao Ati alisema kuwafundisha vijana ufundi kutasaidia kuboresha maisha yao kwani vijana wapo wengi na hawana shughuli maalum wanazozifanya kwa sababu mbalimbali.
Meneja Mradi wa Don Bosco, Badru Juma alisema wamekuwa wakishirikiana na makampuni mbalimbali katika kuwawezesha vijana kupata elimu mbalimbali kwa ajili ya kujikwamua.
Alisema barani Afrika kuna nchi 154 ambazo zina vituo vya Don Bosco na wamekuwa wakishirikiana katika kuondoa changamoto mbalimbali pamoja na kuwakwamua vijana ili waweze kujiajiri ama kuajiriwa.
“ Tumekuwa tukiangalia mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuwawezesha vijana na hivi sasa tumeanzisha utaratibu mpya wa kuboresha mahusiano kati yetu , sekta binafsi, VETA na serikali ili tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini,”alisema Juma.
Post a Comment