TANZANIA na CHINA Kuendelea Kushirikiana Kupitia Utamaduni
Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia), Bw. Clement Mshana pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi. Yang Peili (wa pili kulia) wakifurahia zawadi za vitambaa vilivyonakshiwa na wabunifu wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (kushoto) akipokea zawadi ya kinyago kilichochongwa na wasanii wa Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing (katikati) akifurahia jambo na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana (kulia), akikabidhiwa zawadi ya kinyago.
Hapa ni furaha tupu katika uzinduzi huo.
Waigizaji wa filamu ya’The Young Doctor’ Zhang Yi na Zhou Fang wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015, Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya StarTimes Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga ya Beijing wamezindua maonyesho ya mfululizo wa filamu na tamthiliya mwaka 2015 ambayo yatajumuisha filamu na tamthiliya za kusisimua za kichina barani Afrika.
Kuendelea kwa kukua kwa muingiliano wa tamaduni baina ya watu wa Tanzania na China kumefanya filamu na tamthiliya za China kwenye luninga zijizolee umaarufu mkubwa na kuwa kichocheo kikubwa katika kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga, Bi. Yang Peili amebainisha kuwa Tanzania itabaki kuwa mshirika wake mkubwa na wataendelea kuimarisha mahusiano yao ya kitamaduni kupitia matangazo ya maudhui ambayo yana nafasi ya kipekee kuwafikia watu wengi zaidi.
”Maonyesho haya ambayo kwa kawaida yatakuwa ni ya filamu na tamthiliya kutoka Beijing kwa kiasi kikubwa yataonyeshwa nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa makadirio, jumla ya filamu na tamthiliya 30 za kwenye luninga zitaonyeshwa nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Dhumuni kuu ni kuimarisha muunganiko wa maingiliano ya kiutamaduni baina ya marafiki zetu wa Afrika na watu wa China.” Alisema Bi. Peili
Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga itatoa fursa ya kipekee kwa watazamaji wa barani Afrika kama vile Tanzania, Kenya na Afrika ya Kusini kukutana na washiriki maarufu wa filamu ya ‘The Young Doctor’. Pia wakurugenzi wa mamlaka hiyo watakuwa na wasaa wa kuzungumza na kuyahoji makampuni ya kimataifa ya uzalishaji wa vipindi barani Afrika kwa nchi hizo tatu.
Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ukuaji wa kasi wa tasnia ya filamu na tamthiliya kwenye luninga na kunufaisha maisha ya watu huku masoko ya tasnia hizo kwa nyumbani yakijulikana kimataifa na kuwa kiungo muhimu katika kukuza muingiliano wa kiutamaduni baina ya nchi husika.
Kama sehemu ya chombo cha uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015, sherehe za uzinduzi zitafanyika nchini Afrika ya Kusini ambapo zitahudhuriwa na mamlaka ya bodi hiyo ya Beijing.
“Maonyesho haya yanafuatilia tukio kama hili ambalo lilifanyika mwaka jana na kuandaliwa na Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga ambapo Mr. Guo Jinlong, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mamlaka ya Kisiasa ya CPC na Katibu wa Kamati ya Mamlaka ya Beijing alihudhuria sherehe ya aina yake alipotembelea nchini Tanzania,” alisema Bi. Peili na kumalizia, “Tamthiliya hizi za Kiingereza za kwenye luninga kama zinavyojulikana miongoni mwa watazamaji wengi zimejizolea umaarufu mkubwa burudani inayopendwa katika nchi nyingi za kiafrika na tunaamini kwa pamoja tunaweza kuziunga mkono tasnia za uzalishaji wa vipindi za nyumbani katika nchi husika ili kuweza kunufaika zaidi kwa pande zote mbili.”
Uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015 utajumuisha vipindi vya luninga maarufu na filamu kama vile ‘The Young Doctor’, ‘The Sweet Burden’, ‘The Mi Family’s Marriage’, ‘Ordinary World’, ‘Love is Not Blind’, ’20 Once Again’, ‘A Wedding Invitation’, na ‘The Left Ear’ambazo zimepangwa kuonyeshwa nchini Tanzania ndani ya kipindi cha mwaka mzima.
Shughuli za kukuza maonyesho haya katika nchi zingine za barani Afrika zikiwemo Kenya na Afrika ya Kusini zitafuatia kulingana na kampuni ya matangazo ya dijitali ya StarTimes ambayo ina mpango wa kuzionyesha kupitia katika ving’amuzi vyao vya antenna na madishi, na kwa uhakika itasaidia kwa kiasi kikubwa itasaidia kukuza utamaduni wa China barani Afrika.
Post a Comment