Header Ads

Siku ya Watoto wenye Mtindio wa Ubongo Kufanyika Oktoba 7, 2015

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (Chawaumavita), Hillar Said (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Watu, Watoto wenye mtindio wa ubongo yatakayofanyika, Oktoba 7, 2015 viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa chama hicho, Mwanahamisi Hussein.
 Katibu wa chama hicho, Mwanahamisi Hussein (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo (Chawaumavita) kimewataka wakina baba kuacha tabia ya uoga ya kukimbia majukumu pindi wanapopata watoto wenye ulemavu.

Katika hatua nyingine chama hicho kimewaomba wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kuzungumzia namna gani watasaidia walemavu katika mikutano yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Watu na Watoto Wenye Mtindio wa Ubongo ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 7. Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Hilal Saidi, alisema watoto wenye matatizo hayo wanapaswa kusaidia badala ya kuwatenga.

Alisema kuwa  katika tafiti walizofanya wamegundua kuwa wanaume wengi ni waoga wa majukumu pindi wanapopata watoto wenye ulemavu hadi kupelekea kukimbia famia zao.

"Wanaume wengi waoga wa majukumu hasa anapozaliwa mtoto mwenye ulemavu, wanaona kuwa ni mkosi mkubwa na kuanza kupata msukumo katika familia yake kuachana na mkewe hivyo anateleleza familia huku mwanamke akibaki peke yake" alisema Said

Hata hivyo alisema ulemavu umegawanyika katika makundi matatu ambayo ni  ni ulemavu wa akili,mtindio wa ubongo na viungo.

Alisema watoto wenye ulemavu wa viongo na mtindio wa ubongo wanaweza kupatiwa matibabu hali yao ikawa sawa kushiriki katika katika elimu na kufikia malengo yao.

Hivyo aliwataka wakina baba na familia kwa ujumla kutowafungia ndani watu wenye ulemavu na badala yake kuwapeleka katika vituo vya afya kwaajili ya matibabu na miili yao ikatengemaa.

No comments

Powered by Blogger.