Timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, yakabidhiwa Mipira kwa ajili ya Kujifua zaidi
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum (wa tatu kushoto) na wenzake wakichezea mpira kujaribu viwango vya mipira hiyo baada ya kukabidhiwa na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, suleiman Kova (wa pili kulia), wakati wa mazoezi ya timu ya Kamati ya Amani inayoundwa na Viongozi wa Dini. Mazoezi hayo yalifanyika leo asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, sambamba na timu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zaoTanzania,kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wakirafiki kati yao unaotarajia kuchezwa hivi karibuni.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) akimkabidhi mpira Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, Skei Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Alhad Mussa Salum, baada ya mazoezi ya timu hiyo na timu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Nchini, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini leo asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki unaotarajia kuchezwa hivi karibuni.
Mazoezi ya pamoja...
Mazoezi ya pamoja...
Suleiman Kova, akisalimiana na Mabalozi baada ya kuwakabidhi mipira leo asubuhi.
Picha ya pamoja ya Timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini na Mabalozi baada ya mazoezi yao ya pamoja yaliyopigwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar leo asubuhi.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, akijaribu kumpiga chenga Balozi wa Denimark, wakati wa mazoezi yao ya pamoja kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki.
Mazoezi ya Viungo.....
Nahodha akizungumza na wachezaji wake baada ya mazoezi.
Majadiliano baada ya mazoezi...
Picha na www.sufianimafoto.com
Post a Comment