Serikali yawatembelea Wakimbizi, walioko Kambi ya Nyarugusu Mkoani KIGOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akizungumza na watumishi
mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya
wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo
ina hifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) na Burundi.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (kushoto)
akizungumza na watumishi wa mashirika mbalimbali yaliyoko katika kambi
ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma (hawapo
pichani) wakati waziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) aliyetembelea kambi hiyo jana.
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akiongozana na Mkuu wa
Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu (B),Fredrick Nisajile(kulia) na Mkuu wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) ofisi ya
Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya Katibu
Mkuu katika makazi ya wakimbizi yaliyopo Nyarugusu wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ,akimsikiliza mmoja wa maofisa wa
Shirika la Chakula Duniani (WFP) alipotembelea ndani ya mahema
wanakoishi wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), akiongozana na Mkuu wa
Kambi ya Nyarugusu (B),Fredrick Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah
Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kambini
hapo jana. Kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ina
hifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na
Burundi.
Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja
wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Amah
Assiama-Hillgartner ( kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil (katikati), aliyetembelea
hospitali hiyo wakati wa ziara yake katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu.
Daktari wa Hospitali ya Kambi ya
Wakimbizi ya Nyarugusu, Florence Mshana (aliyeshika karatasi),akitoa
taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mbarak
Abdulwakil (kushoto), alipotembelea hospitali hiyo wakati wa ziara yake
ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma. Kambi hiyo ina hifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Post a Comment