Header Ads

Siku ya Kujitolea Duniani yafanyika Nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel aliyevaa suti akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Bi Ritha Mushi (VSO Volunteer) akiongea na Vijana wenzake juu ya umuhimu wa kujitolea katika kongamano la siku ya kujitolea duniani lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kijana akipata maelezo juu ya utendaji kazi wa shirika lisilo la Kiserikali la JICA wakati wa kongamano la siku ya kujitolea lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa  maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Dr Ven kutoka DFID akiwaasa vijana  wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa  maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Bw. Ian Tarimo anaejitolea katika Shirika lisilo la Kiserikali la Youth For Change akiongea na Vijana  wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea katika taasisi mbalimbali wakati wa  maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kulia akiongea na wanahabari katika maadhimisho ya siku ya kujitolea duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Overseas (VSO) Dkt. Philip Goodwin.

No comments

Powered by Blogger.