Mhandisi
wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Paul Magembe akitoa maelezo kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu mitambo ya
kutolea huduma za kifedha iliyopo katika ofisi za Kampuni hiyo mkoani Dodoma.
...............................
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL) kujipanga na kuanza mkakati wa kutangaza huduma za fedha ambazo
zitatolewa na kampuni hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Prof.
Mbarawa ametoa agizo hilo baada ya kukagua mitambo itakayotumika kwa huduma
hiyo ambayo itaongeza ushindani wa biashara kwenye huduma za simu nchini mkoani
Dodoma.
"Lazima
mjipange kwenye idara ya masoko kwa kuanza kutangaza huduma hiyo kupitia njia
zote zikiwemo mitandao ya kijamii, ili wananchi warahisishiwe huduma za fedha
kupitia TTCL", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha,
ameiagiza kampuni hiyo kupitia idara ya masoko kujipanga kuona fursa zilizopo
kwa kufahamu mahitaji ya wateja wao na kuhakikisha inaongeza wateja
katika mkoa huo ili kuteka soko la ushindani ambapo Serikali inajipanga
kuhamia huko.
Waziri
Prof.Mbarawa ametaja baadhi ya maeneo ambayo TTCL inahitaji kuboresha zaidi ni
upande wa Simu (Voice) na Data (video) ili kuweza kurahisisha mawasiliano
kwa njia ya video conference kwa kuwa kuna baadhi ya watendaji wengine
watabaki Dar es salaam.
|
Post a Comment