Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Idara na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Manyoni (hawapo pichani) juu ya uwajibikaji kwa vitendo na sio kwa mazoea ili kuleta ufanisi sehemu za kazi walio kaa kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya Manyoni Geoffrey Mwambe, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manyoni Moses Matonya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Edward Fussi. ......................................
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara katika halmashauri mpya ya
Itigi na Manyoni huku akibaini uwepo wa changamoto mbalimbali hususan
upungufu wa dawa katika Kituo cha Afya Itigi na Hospitali ya wilaya ya
Manyoni mkoani Singida.
Akizungumza katika ziara hiyo, Jafo amesema mara baada ya kutembelea
Halmashauri hizo amebaini changamoto za dawa katika kituo cha afya
Itigi pamoja na vifaa katika chumba cha mama huku akisema zipo
changamoto ambazo zinazotakiwa kutatuliwa ndani ya halmashauri hiyo.
Jafo akizungumza kuhusu suala la upatikanaji wa dawa, amesema tatizo
hilo linaonekana ni kikwazo kutokana na watendaji kushindwa kutumia
fedha za dharura wanazopewa na serikali kununulia dawa na vifaa tiba.
“Naziagiza Halmashauri hizi kuhakikisha zinaweka kipaumbele uboreshaji
wa vituo vya afya kwa kununua dawa nyingi na vifaa vingine tofauti na
kusubiri zinazotoka Bohari ya Madawa (MSD),”amesema Naibu Waziri huyo
|
Post a Comment