Wataalamu wa afya wa Hopsitali ya Mt Meru ya Jijini Arusha wakiwa katika maandalizi ya kufanikisha zoezi la kutoa damu kutoka kwa wachangiaji ambao walijitokeza jana kusaidia upungufu uliopo hospitalini hapo, Wengine pichani ni baadhi yaviongozi na wanachama wabaraza la vijana la CHADEMA wilaya ya Arusha Mjini waliojitokeza kuchangia damu kwa hiyari.
..................................
Vijana kutoka Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Arusha Mjini wakiungwa mkono na baadhi ya wananchi wengine wamefanya zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia hospitali yaMt Meru inayokabiliwa na upungufu mkubwa wa damu hali inayochangia ongezeko la vifo hasa akina mama wakati wa kujifungua.
Akizungumza jana katika katika Hopsitali ya Mt Meru, mratibu wa zoezi hilo kwa upande wa wachagiaji, Katibu wa BAVICHA Wilaya ya Arusha Mjini ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Glory Kaaya alisema zoezi hilo limefanyika maalum kama tukio la kuaga mwaka huu wa 2016 kwa kuwahamsiaha vijana wenzake na wanajamii wengine kujitolea kuchangia na kusaidia kupunguza upungufu wa damu katika hospitali ya Mt Meruwakiamini mchango wao utasaidia kuokoa maisha ya watu wengi.
Miongoni mwa watu mashuhuri waliojitokeza kuunga mkono zoezi hilo ni pamoja na Mbunge wa Simanjiro Mh James Olemiya, Naibu Meya Jiji la Arusha Viola Likindikoki pamoja na baadhi ya madiwani wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha akiwemo Ddiwani Ephata Nanyaro wa Kata ya Levolosi na Rick Moiro wa Kata ya Moshono.
|
Post a Comment