Timu ya Kijitonyama Veterans yapata Viongozi Wapya
Timu ya Kijitinyama Veterans yenye maskani yake
Kijitonyama, leo imefanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi wapya wa kuingoza
timu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni tisa, ambapo katika
nafasi ya Mwenyekiti aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo muda uliopita, Lupyana
Michael, ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura na wajumbe
na kuongoza dhidi ya mpinzani wake, Petro Malima .
Pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Timu hiyo Amon Petro,
naye ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka na kura nyingi zaidi
ya mpinzani wake, Evodius Mtawala
Naye Mratibu wa timu hiyo, Majuto Omary,pia ameendelea
kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka kidedea dhidi ya mpinzani wake Evans
Malla,
Kwa mujibu ya utaratibu wa Timu hiyo, kutokana na
mapendekezo ya Wajumbe, katika uchaguzi, majina mawili yanayopigiwa kura na
mmoja kati yao anayepata kura nyingi ndiye anapaswa kuwa kuwa kiongozi katika
nafasi husika na anayefuatia kwa kura anakuwa msaidizi.
VIONGOZI WALIOCHAGULIWA:-
MWENYEKITI: Lupyana Michael
MAKAMU MWENYEKITI: Malima Petro
KATIBU MKUU: Amon Petro
KATIBU MSAIDIZI: Evodius Mtawala
MRATIBU MKUU: Majuto Omary
MTARIBU MSAIDIZI: Evans Malla
MWEKAHAZINA MKUU: Othaman Hussein
MWEKA HAZINA MSAIDIZI: Sweetbert Mwombeki
MSEMAJI WA TIMU: Muhidin Sufiani (Mafoto)
Baadhi ya wajumbe
wakipitia vifungu vya katiba wakati wa uchaguzi huo.
Post a Comment