Serikali Yatangaza Rasmi Kuitambua Mitandao ya Kijamii ( BLOGGERS )
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.
....................................................
....................................................
Na Dotto Mwaibale
Serikali imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Bloggers) kuwa chombo cha habari nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas Dar es Salaam leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN).
"Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali" alisema Abbas.
Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.
Katika hatua nyingine Abbas alisema Bloggers haina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weredi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine.
Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.
Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa 'Press Card' jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.
Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kulia), akizungumza katika mkutano huo kuhusu masuala mbalimbali ya benki hiyo ambayo ni moja ya mdhamini wa mkutano huo.
Mwanahabari na Blogger Frederick Katulanda (kulia), akiuliza swali.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (kushoto), akiwaelekeza jambo mablogger.
Mablogger wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mablogger kazini..
Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence Mello akitoa mada.
Meza kuu. Kutoka kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Kranty Mwantepele.Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi pamoja na Katibu wa muda wa TNB, Khadija Kalili.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (katikati), akizungumza kwenye mkutano huo.
Bloggers wakifuatilia mada.
Blogger Mroki Mroki akiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Mgeni rasmi akihutubia.
Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo, Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel Seria (kulia), akiuliza swali,Kushoto ni William Malecela mmiliki wa mtandao wa Mwananchi na katikati ni mmiliki wa Blog ya Michuzi Issa Michuzi.
Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja...
Post a Comment