CHADEMA yatoa Elimu Kwa Viongozi wa Mabaraza Wilaya ya Nyamagana, Mwanza
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Lengo lilikuwa ni kuimarisha mabaraza hayo kwa ajili ya utendaji kazi wake ikiwemo kuhakikisha wanachama wapya wanaendelea kujiunga na chama chadema ili kukifanya kuendelea kuwa chama cha upinzani chenye nguvu nchini.
Chama hicho kililaani zoezi la kuwahamisha machinga kutoka katikati ya Jiji la Mwanza huku mazingira rafiki yakiwa bado hayajaandaliwa ambapo Micus alisema hatua hiyo inaweza kusababisha vijana na akina mama wengi kukosa mwelekeo wa kujitafutia kipato kwa njia sahihi ambapo walihimiza machinga hao kutengenezewa mazingira bora ya kufanyia biashara zao.
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Diwani wa Kaya ya Butimba, John Pambalu, akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza diwani wa Kata ya Butimba, John Pambalu, wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana, wakifuatilia kwa makini semina iliyotolewa kwa ajili ya kuimarisha uhai katika utendaji wao wa kazi ili kujiimarisha zaidi.
Post a Comment