Watanzania Wahimizwa Kuchangia Damu Kwa Hiyari Kuokoa Maisha
Makamu
wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na
mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi
la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi
hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la
Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa
wiki.
Makamu
wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa vipimo na
mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kulia) wakati wa zoezi
la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi
hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiyari lilifanyika eneo la
Karume jijini Dar es Salaam kwa siku mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa
wiki.
Mfanyakazi
wa Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed (kushoto)
akimfanyia vipimo mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwa hiyari
wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura
hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Makamu
wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa
Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya
kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa
hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la
Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi.
Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa
ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha
Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakifanyiwa vipimo
katika zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akipimwa presha kabla ya kushiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa mkazi wa Dar es Salaam akishiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
..............................
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kitengo cha dharura
wametoa rai kwa watanzania kujitolea kwa hiyari kuchangia damu ili kuokoa
maisha ya wagonjwa wanaopokelewa hospitalini hapo.
Akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika
kwa siku mbili mwishoni mwa wiki katika eneo la Karume jijini Dar es Salaam,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru
amebainisha kuwa zoezi hilo ni muhimu sana kwani litasaidia kuokoa maisha ya
wagonjwa wenye uhitaji huo wanaopokelewa hospitalini hapo kama vile waliopata
ajali, wakina mama wajawazito na watoto.
“Hospitali ya Taifa Muhimbili inahitaji
wastani wa chupa za damu 100 lakini tunafanikiwa kupata wastani wa chupa 40
hivyo kuwepo na upungufu wa chupa 60 kila siku. Hali hii inapelekea kuhudumia
wagonjwa wenye uhitaji wa dharura tu huku wengine wakisubiri.” Alisema Profesa
Maseru
“Wataalamu wananiambia kuwa kwa
kawaida, damu inaweza kuhifadhiwa kwa muda wa takribani mwezi mzima kabla ya
muda wake wa kutumika kwisha, na kutokana na uhifadhi wa damu kwa muda mfupi
ndiyo maana tunasisitiza umuhimu wa watu kuchangia mara kwa mara.
Kitaalamu mwanamume anaweza kuchangia mara nne kwa mwaka na mwanamke mara
tatu kwa mwaka.” Aliongezea Profesa Maseru
“Katika wakati wa kutoa huduma ya
tiba ya dharura, haswa kwa wagonjwa wa ajali, watoto na wamama wajawazito,
upatikanaji wa huduma ya Ambulance na damu kwa wakati huongeza nafasi ya
kuishi kwa wahitaji kwa kiasi kikubwa mno na huduma hizi huokoa maisha ya
mamilioni ya wagonjwa kila mwaka duniani kote,” alisema na kumalizia,
“Natoa rai kwa wakazi wa Dar es slaaam na Watanzania wote kwa ujumla
kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili nchi iwe na akiba
ya damu ya kutosha, kwani asilimia moja ya Watanzania wakiamua kuwa wachangiaji
damu wa kujirudia Mpango wa Taifa wa Damu Salama utaweza kukidhi
mahitaji ya damu nchini.”
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa
StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif, kampuni inayojishughulisha na uuzaji na
usambazaji wa ving’amuzi kwa ajili ya matangazo ya dijitali ambao walidhamini
zoezi hilo amesema kuwa hii ni mara ya pili wao kudhamini zoezi hilo kutokana
na umuhimu wake katika kuokoa maisha ya watanzania wote kwa ujumla.
“Hakuna asiyefahamu katika maisha
yetu yanayotuzunguka ajali zimekuwa nyingi zinazopelekea watu kupoteza maisha
maelefu kubaki mejeruhi wenye uhitaji mkubwa wa damu ili kupata matibabu. Kama
tunafuatilia vyombo vya habari basi tutakuwa tunasikia ni mara ngapi kwa wiki
ajali zinatokea barabarani na kuacha majeruhi wengi. Kwa upande wa akina mama
wajawazito wanahitaji damu kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kujifungua.
Hatuwezi
kukaa pembeni na kuwatizama wakikosa msaada wakati uwezo huo tunao.” Aliongezea
Bi. Hanif
“Tumejisikia faraja sana kuwa
wamojawapo wa wadau walioshiriki kufanikisha zeozi hili na tunaahidi kuendelea
kushirikiana na Muhimbili katika kuwahamasisha watanzania wajitokeze zaidi.
Kwa
mujibu wa wataalamu tunaweza kujitolea damu mpaka mara nne ndani ya mwaka, nina
uhakika kila mtanzania akifanya hivyo basi benki yetu ya damu itajaa na
tutaweza hata kusaidia wengine wa nchi za jirani wenye uhitaji.” Alimalizia
Makamu wa Rais kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania.
Post a Comment