Header Ads

Mkutano wa Wadau wa Takwimu wafanyika Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akihutubia wakati akifungua mkutano wa wadau wa takwimu Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolph Mkenda na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa. Mkutano huo uliandaliwa na NBS.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa akihutubia kwenye mkutano huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolph Mkenda  akizungumza katika mkutano huo.

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Dk.Rogers Dhliwayo akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masula ya Uchumi na Kijamii (ESRF), Oswald Mashindano (Ph.D), akizungumza katika mkutano huo.
Muongozaji wa mkutano huo, Maria Sarungi akitoa maelekezo.
Wadau mbalimbali wa masula ya takwimu wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Viongozi wakiwa Meza kuu.
Washiriki kutoka mashirika ya maendeleo ya kimataifa wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amewataka watendaji wa Serikali kutoa takwimu mbalimbali za maendeleo na kuziweka katika mitandao ili wananchi waweze kuziona na kuhoji mipango ya maendeleo iliyofanyika hama kukwama.

Hayo aliyabainisha wakati akifungua mkutano wa wadau wa takwimu ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kukubaliana jinsi ya kushirikiana katika kuhakikisha takwimu za viashiria vya Mpango wa Maendeleo Endelevu zinapatikana kwa wakati. 

Alisema takwimu mbalimbali ni lazima zioneshe mipango ya maendeleo iliyofanyika au kumalizika badala ya kuwa siri na kuwafanya wananchi kushindwa kuhoji.

"Takwimu mbalimbali za maendeleo zikiwa wazi itasaidia wananchi kufahamu miradi ya maendeleo iliyopo na iliyokwama jambo ambalo litasaidia kusukuma maendeleo ya nchi" alisema Sefue.

Alisema lengo la  lengo la kuelimishana juu ya kukamilika kwa utekelezaji wa Malengo ya Milenia (MDGs) na kuanza kwa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu - Sustainable Development Goals (SDGs).


Aliongeza kuwa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia - MDGs ulikuwa ni wa miaka 15 kuanzia mwaka 2000 hadi 2015. Mpango huu wa MDGs unakamilika mwaka huu na kuanza kwa mpango mpya wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambao pia ni miaka 15 ijayo.

Alisema Tanzania ni nchi ya kwanza kuanza kufanya vikao vya kutekeleza mpango huo wa maendeleo jambo ambalo linaonesha kuwa na kasi ya kuyafikia maendeleo hayo ya dunia.

Mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ulihudhuriwa na wadau wa takwimu takribani 100 kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Wadau wa Sekta Binafsi pamoja na Wadau wa Taasisi za Elimu ya Juu.


Septemba mwaka huu, viongozi wa nchi mbalimbali duniani akiwemo Rais Jakaya Kikwete walikutana nchini Marekani kwa ajili ya kutathmini utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia – MDGs ambapo ilionekana kwamba kuna baadhi ya malengo yalikuwa yamefanikiwa na mengine hayakufanikiwa.

No comments

Powered by Blogger.