Jaji DAMIAN LUBUVA amtangaza Dkt JOHN MAGUFULI kuwa Rais Mteule wa TANZANIA
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya
Taifa Jaji Damian Lubuva akifafanua baadhi ya mambo mapema leo jioni
kabla ya mawakala wa vyama kusaini fomu namba 27 iliyosainiwa na
mawakala wa vyama vya siasa baada ya majumuisho ya kura kwa wagombea
urais kabla ya kutangaza rais mteule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
ambapo Dk. John Pombe Magufuli ametangazwa mshindi kwa kura kura
8.882.935 sawa na asilimia 58.46 huku mpinzania wake kutoka Umoja wa
Vyama vya Upinzani kupitia chama cha Chadema Edwald Lowasa akipata kura
6.072.848 sawa na asilimia 39.97.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya
Taifa Jaji Damian Lubuva akisaini fomu namba 27 mara baada ya mawakala
wa vyama vya siasa kusaini kabla ya kumtangaza rasmi rais mteule kwenye
ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam leo ambapo Dk. John Pombe Magufuli
ametangazwa kuwa rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushoto
ni Mkurugenzi wa Tume hiyo Ndugu Kailima Ramadhan na kushoto ni Jaji
Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya
Taifa Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu
Mkuu wa CCM nakala ya fomu namba 27 ambayo mawakala wa vyama wamesaini
mara baada ya kukamilisha majumuisho ya kura za wagombea urais kabla ya
kutangaza matokeo mapema leo katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Hamid Mahmod.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya
Taifa Jaji Damian Lubuva akitangaza matokeo hayo kwenye ukumbi wa JNICC
jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya mawakala na viongozi wa
vyama mbalimbali vya siasa waliohudhuria kushuhudia matangazo hayo
yaliyokuwa yakitolewa na tume ya uchaguzi ya taifa leo kwenye ukumbi wa
kimataifa wa JNICC jijini Dar es salaam.
Maofisa mbalimbali wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na serikali wakifuatilia matangazo hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana pamoja na wageni mbalimbali wa ndani na nje
waliohudhuria ili kushuhudia Rais mteule akitangazwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
Assa Mwambene Mkurugenzi wa Idara
ya Habari Maelezo na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali TSM
Gabriel Nderumaki wakijadili jambo wakati wakisubiri kuanza kwa utiaji
saini kwa mawakala wa vyama vya siasa kwenye fomu namba 27 kabla ya
kutangaza matokeo ya jumla ya wagombea urais wa Tanzania.
Baadhi ya mawakala wakipitia fomu namba 25 na 26 kabla ya kusaini fomu namba 27.
Baadhi ya mawakala wakisaini fomu hizo.
Post a Comment