Mazishi ya Dkt EMANNUELMAKAIDI kufanyika Makaburi ya SINZA, Jijini Dar es Salaam
Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi akiwa katika huzuni baada ya kuondokewa na mpendwa wake.
Mtoto wa kwanza wa Dk. Makaidi, Hilda Emmanuel Makaidi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ratiba ya mazishi ya baba yake.
Ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa Dk.Makaidi Sinza.
Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi (kulia), akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwake Sinza Vertican Dar es Salaam kesho asubuhi.
Na Dotto Mwaibale
MWILI wa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanueli Makaidi unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi alisema mwili huo baada ya kutoka Masasi ulipelekwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na leo jioni utapelekwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza Vertican ambapo itafanyika ibada fupi na kupata fursa ya ndugu na majirani kuuaga.
Alisema kesho mwili huo utaagwa katika viwanja vya Karimjee ambapo viongozi mbalimbali wa kisiasa, serikali watakuwepo na kisha kufanyika mazishi yake katika makaburi ya Sinza.
"Unajua baba alikuwa ni mwanasiasa na amefariki akiwa bado ni mwanasiasa hivyo ni lazima uweze kuagwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali" alisema.
Akimzungumzia baba yake alisema marehemu alikuwa ni mtu ambaye anapenda utu ambapo alipenda kila binadamu ni sawa na hapaswi kubaguliwa.
Alisema wameamaua kumzika baba yao Dar es Salaam na si Mtwara kutokana na mke na mama yake kuzikwa Dar es Salaamna ndio utaratibu waliouweka wa kuzikwa.
"Baba alitaka kila mtu ambaye atafariki ni vyema akazikiwa hapo kwani hata wakati wa kulimia makaburi inakuwa rahisi,"alisema.
Kwa upande wake mtoto wa pili wa Marehemu Hilda Makaidi alisema baba yao alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu.
"Nakumbuka nilimpigia baba simu akiniambia mwanangu Hilda Masasi kugumu, na mimi nikamwambia baba rudi nyumbani tukutibu lakini hakukubali haraka,"alisema.
Alisema baba ameacha mjane na watoto 10 huku ikiwa wakike wakiwa wanne na wakiume sita na wajukuu 10 na vitukuu sita.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi George Kahangwa alisema mazishi hayo yatahuduliwa na mgombea urais wa umoja huo Edward Lowassa pamoja na viongozi wa taifa wa serikali na vyama vya siasa na vyama vya michezo.
"Sote tushiriki kumpa heshima za mwisho na kumsindikiza mpendwa wetu katika safari ya mwisho,"alisema.
Post a Comment