Wenyeviti wa Tume za Uchaguzi wa Nchi za Afrika Mashariki Waisifu NEC
Na Mwandishi Wetu
Tume za Uchaguzi katika Jumuia ya Africa Mashariki zimetakiwa kushirikiana na kutoa ushirikiano kwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanziba (ZEC) katika
kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Hayo
yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Africa Mashariki Bwana
Charles Njoroge wakati wa ufunguzi wa mkutano wa forum ya viongozi wa
Tume za Uchaguzi za Jumuia hiyo uliofanyika katika hoteli ya New Africa
Hoteli jijini Dar es Salaam leo.
“Uenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ni nafasi nyeti na ina changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kijamii na kisiasa ,
ni matumaini yangu kwamba iwapo tutaungana na kufanya kazi pamoja
jumuia ya Africa Mashariki Forum na kushirikiana kuweka nguvu katika
kuendesha chaguzi kutakuwa na ufanisi , uhuru na haki katika chaguzi zetu na kufikia malengo tunayoyataka” Alisema Njoroge.
Uchaguzi
nchini Tanzania mwaka huu umekuwa na hamasa kubwa ukilinganisha na
chaguzi zilizopita katika nyanja mbalimbali ikiwepo ushiriki wa wananchi
na idadi ya wagombea imekuwa kubwa, hii inathihirisha kuwa wananchi
wamekuwa na uelewa mkubwa na wanatambua haki zao na kuitaka serikali
iwajibike kwao.
Aidha Njoroge amezitaka
tume za jumuia ya Africa Mashariki kufikiri kwa kina na kuweka mikakati
ambayo itasaidia kupunguza gharama za Uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuandaa sera ya kusaidiana katika vifaa vya uchaguzi.
Viongozi
hao wa Tume ambao wameitembelea Tanzania chini ya Mwenyeji wao ambaye
ndiye mwenyekiti wa umoja huo wa Tume za Uchaguzi za Jumuia ya Africa
Mashariki na ndiye mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva
walitembelea kitengo cha Daftari ambapo walijionea namna taarifa za
Mpiga Kura zinavyoingizwa katika mfumo wa Daftari.
Wakiwa katika ziara hiyo Kamishna wa Tume huru ya Uchaguzi ya KenyaBalozi
Mohamed Alawi ameipongeza Tume ya Uchaguzi ya Tanzania kwa kazi kubwa
na nzuri iliyofanya kwa kuda mfupi imeweza kuandikisha wapiga Kura
milioni ishirini na nne kwa
kutumia BVR elfu nane (8,000) ukilinganisha na nchini mwake ambapo
walikuwa na BVR 15,000 na waliweza kuandikisha wapiga Kura milioni kumi
na tano kwa muda mrefu.Ikiwa ni pamoja na kuliweka wazi Daftari la awali la mpiga Kura mapema kuliko ilivyofanyika nchini kwao.
Aidha balozi Alawi aliongeza kuwa Uchaguzi ni zoezi kubwa katika nchi,haliwezi
kuachiwa NEC pekeyake, kama inavyosemwa vita haiwezi kupiganwa na
majemedali pekee, Uchaguzi ni zoezi linalofanywa na watanzania wote kwa
ujumla, kwa maana hiyo ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa na
wagombea wao wasitoe matamshi ambayo yatajenga chuki miongoni mwa jamii/
wapiga kura, tunafahamu watanzania ni wakomavu kisiasa, ni watu
watulivu waitunze amani waliyonayo kwani Tanzania ipo kabla ya Uchaguzi,
wakati wa Uchaguzi na baada ya Uchaguzi.
Viongozi hao ambao wamekuja nchini kujiridhisha na maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa unaotarajia kufanyika mwezi ujao wa wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni kukemea vyama
vya siasa vinavyokiuka maadili ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutoa
matamshi ambayo yanaweza kujenga chuki miongoni mwa Watanzania.
Post a Comment