Wadau wa Elimu Kukutana Jijini ARUSHA kujadili namna ya Kuinua Kiwango cha Elimu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeandaa Kongamano la
siku mbili la Elimu ya Juu litakalofanyika jijini Arusha kwa lengo la kuwa na
jukwaa la kubadilishana uzoefu na maarifa miongoni mwa wadau wa elimu nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu
nchini (TCU) Prof. Yunus Mgaya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam .
Amesema Kongamano hilo litaenda sambamba na Maonesho ya
shughuli mbalimbali zikiwemo za utoaji wa huduma, na maonesho ya bidhaa
mbalimbali kuonyesha mafanikio ya elimu
yaliyopatikana nchini.
Amesema washiriki wa mkutano huo kutoka taasisi mbalimbali
watapata fursa ya kuchangia miradi elimu kwa ili kuinua sekta hiyo hapa nchini.
“Tunatarajia kuweka mikakati itakayowezesha kuwa na
ushirikiano madhubuti baina ya Taasisi za Elimu ya Juu na Sekta Binafsi ili
kubaini fursa na changamoto zilizopo tukilenga kuchochea maendeleo na kukuza
ajira kwa wahitimu wetu ”, Alisema Prof.Mgaya.
Amefafanua kuwa Kongamano hilo la siku mbili litafanyika
mnamo tarehe 1 hadi 2 Oktoba2015 katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha
likiongozwa na Kauli Mbiu isemayo
“Kujenga Uwezo kwa ajili ya uzalishaji na ushinda ni Kitaifa :Matarajio na
changamoto kwa muongo ujao”.
Wizara ya Elimu
imeandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Baraza la
Taifa la Elimuya Ufundi (NACTE) Kamati ya Makamu wa Vyuo Vikuu nchini (CVCPT)
pamoja na wadau wa Elimu ya Juu kutoka
ndani na nje nchi, Watendaji wa Serikali, Sekta Binafsi, Wabia wa Maendeleo,
Taasisi zisizo za Kiserikali, Vyama vya Kitaaluma, Wahadhiri, Chama cha
WaajirinaWanasiasa.
Post a Comment