TWIGA STARS, Kuondoka Hii Leo
Timu
 ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuondoka nchini kesho 
usiku kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye michuano ya Michezo ya 
Afrika (All Africa Games) inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 3,
 mwaka huu.
Kutokana na sababu zilizo nje ya 
uwezo wa TFF, Twiga Stars haikuondoka leo kuelekea nchini Congo – 
Brazzavile, Shirikisho bado linasubiri mwongozo wa Wizara ya 
Habari,Viajana, Utamaduni na Michezo.
Imani ya TFF ni kuwa timu 
itasafiri na kuwahi mechi ili kuepuka hatari ya kuadhibiwa na CAF ikiwa 
ni pamoja nan a kulipishwa fainai au kuondolewa kwenye michuano hiyo.
Mchezo wa kwanza wa Twiga Stars 
katika michuano hiyo  utakua dhidi ya Ivory Coast tarehe 6, Septemba, 
mchezo wa pili dhidi ya Nigeria Septemba 9 na mchezo wa mwisho katika 
kundi hilo utakua dhidi ya      Congo-Brazzavile Septemba 12, 2015.
Timu mbili kutoka kundi A zitaungana na timu mbili nyingine kutoka kundi B kucheza hatua ya nusu fainali.

Post a Comment